Kwa nini usachi simu ya mpenzio?


Big up mkuu, nakubaliana na wewe mia kwa mia lazima kujua status ya mwenzako. na lakini kwa nini mfichane?
 
Big up mkuu, nakubaliana na wewe mia kwa mia lazima kujua status ya mwenzako. na lakini kwa nini mfichane?

Remmy, unaijua status ya mpenzi wako/mumeo/mkeo kwa kuchunguza simu yake?
 
Siipendi kabisa simu ya mke wangu.
Ile ni simu yake ya mkononi, siishiki, pia sitaki aishike yangu.
Namuamini kuwa ni msafi, binafsi najiamini pia..
Akitaka kunionyesha kitu, basi atanipa yeye mwenyewe, na sitavuta mipaka.

kama mnapenda na mliambana mtakuwa pamoja kwenye shida na raha
nini simu kitu gani???mwache achungulie kama msafi wa ndoa/uhusiano wako akuna atakacho kumbana nacho zaidi ataishia kucheka na ku smile ,..n hiyo kumwakikishia usalama wake zaidi....
 

si kweli acha tusiwadanganye watu....mi nikiwa na mpenzi wa aina hiyo kwanza nafurahi ukiona mwenzio anashika simu yako anakupenda
anakutakia mema,...si wote wenye nia ya ubaya wengine wanajua simu vishawishi so wanakusaidia ahata wakikufuma na masg zako za sweetbaby,hny darling,mnaitana mnarekebishana unakuwa umemwokoa na umeokoa uhai wa watoto zako...kwa nini uzae mtoto anaumwa wakati kuna uwezekano wa ku avoid???matapeli wa mapenzi wengi waoga kushikwa simu zao...ukiona mkeo ama mumeo anashika simu yako mwongezee na dollar kabisa...
 

pole sana mzee, yamekukuta nn?
mbona unaogopa sana mpenzi wako asione kilichoko katika simu yako?.....kuna nini cha siri wakati ukiugua ndiye atayekutawaza? Wanaojilisha upepo kumbe wako wengi! masha yamekuwa mafupi sana siku hizi, na asilimia 20 ya wanaume waliooa wanalea watoto wasio wao!!!!! angalia usije kuwa mmoja wao.
 
Siipendi kabisa simu ya mke wangu.
Ile ni simu yake ya mkononi, siishiki, pia sitaki aishike yangu.
Namuamini kuwa ni msafi, binafsi najiamini pia..
Akitaka kunionyesha kitu, basi atanipa yeye mwenyewe, na sitavuta mipaka.

Katika hali kama hii inaonyesha kuwa hata wanandoa wanaopata ukimwi shurti wawe wamelia kwenye wali au juice kwenye cafe fulani manake huku kuaminiana inaonekana ni kukubwa saaaana.
Labda zaidi ya 75% ya wanandoa wanaishi kwa imani tu lakini siyo bayana ya uhalisia wa mambo. Kwamba wanaamini/kufahamu kuwa nyendo kinyume na misingi ipo, lakini wasingetaka kufahamu. Watu wanadanganyana, eti sijui upendo, sijui kuchokana n.k. Hizi simu na mtandao ya internet zimeleta maendeleo makubwa lakini pia zimechangia sana kuharibu ndoa nyingi. Zimeongeza sana tija kwa mafataki.
 
I wouldn't like if my partner start to search my phone in my absence... thats called insecurity... I dont search my partner's phone for one main reason...
I would rather not know if he is having affair, I really dont wanna find out at least not at this moment
 
Kwasababu simu ndio midori ya wakubwa,hivyo yapendeza kuzichezea mara uzionapo,na vile vile zinawekwa hela hivyo ni bora kuzisachi waweza ambulia kitita!!!
sasa wewe unatafuta mkong'oto,akigundua salio lake limehamia kwako?vurugu unaziweza?
 
Kuna wengine huenda mabali zaidi wanapopata nafasi kama hiyo huweka simu kadi zao za ziada na kukopi number kutoka katika simu za wapenzi wao kwa hiyo wanakuwa na wakati mzuri wa kuzifanyia utafiti wakiwa mabali na wapenzi wao .kuna siku Ndugu yangu alitumiwa Text na mtu asie mjuwa na kumuliza wewe fulani ni nani kwako?pale pale nikajuwa kuwa jamaa ni Very sad na ni luza.
 
Kusachi simu ya mwenzio tayari umemvunjia Heshima kwa kumuona kuwa sio Mwaminifu.
Wanawake na Wanaume wapo wenye tabia kama hizo.
Kwa mchezo huo mtaishi maisha ya mashaka na ugomvi hadi mwisho wa maisha yenu.
 
Uchunguzi uliofanyika,katika nchi za kiafrika hivi karibuni, umegundua kuwa, kwa kutahiriwa,mwanamme anapunguza uwezekano wa kuambukizwa ukimwi kwa asilimia hamsini.UJUMBE ; kama una jamaa/ndugu yako bado ana ile sijui wanaita nini? mshauri atoe/akatahiriwe. .
 
Kama kweli watu mi wasafi wa miili na mioyo kuna ubaya gani wa mme au mke kushika simu ya mwenza wake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…