Kwa nini vinywaji type ya "Mo Energy" au "Amaz Energy" vinaongeza ashki ya ngono?

Kwa nini vinywaji type ya "Mo Energy" au "Amaz Energy" vinaongeza ashki ya ngono?

Nobunaga

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2019
Posts
1,205
Reaction score
5,121
Nilikuwa nasikiasikia tuu watu wakisema hivi vinywaji type ya "___ Energy" vinaongeza nguvu ya mwili na ashki ya mapenzi, pamoja na sifa zingine zingine ila nikawa siamini.

Kutokana na maneno maneno mengi kuhusu hizi aina za vinywaji, basi sikuvutiwa navyo sana na niliamua kukaa navyo pembeni na sikuwahi kuvitumia huko nyuma.

Sasa leo bahati mbaya nikawa niko mahali na nina kiu ya soda sana. Muuzaji akawa hana soda nyingine tofauti na hizi Energy. Basi nikapiga moyo konde nikaipiga hivyohivyo kisha nikasepa zangu nyumbani.

Ila sasa mabadiliko ya mwili niliyoyasikia yalikuwa tofauti kabisa na nikinywa soda zingine. Niseme tuu mjuba alisimama kwa fujo, huku mapigo ya moyo yakiongezeka mara dufu bila sababu yoyote ile.

Swali ninalojiuliza hapa ni usalama wa hizi Energy drinks ambazo zinapendwa sana vijana huko mitaani. Serikali hasa TMDA imevifanyia uhakiki wa kutosha kweli kuhakikisha hakuna "Kitu cha nyongeza" kinachowekwa?

VIJANA CHUKUENI TAHADHARI.

Energy.jpg
 
Mtafanya vijama wayafakamie mpaka yaishe stoo,
Maana vijana na hili janga la nguvu za kiume linawapeleka puta,
Nina bwana mdogo wangu anauza saana zile dawa za kikongo na ana soko kweli kweli.

Au ndio maana watu wengi nawaona wanakunywa saana hivi vinywaji 🤔
Hizi energy sio kabisa...

Ni za kukaa nazo mbali..
 
Hizo makitu zinaongeza kasi ya mzunguko wa damu, na hiyo inapelekea usingizi kukata, mishipa kujaa damu na hisia za ngono zinakuja kihivyo. redbull ni mfano tosha, na hivyo vieneji vingine navyo hivyohivyo.
 
Juzi nimetoka nje saa 4 usiku nitafute kinywaji kwa Mangi nikakuta anayoniyo Energy ya Mohamed.

Nikanywa. Aisee sijalala hadi saa 10 alfajiri sina ata lepe la usingizi.
 
Juzi nimetoka nje saa 4 usiku nitafute kinywaji kwa Mangi nikakuta anayoniyo Energy ya Mohamed.

Nikanywa. Aisee sijalala hadi saa 10 alfajiri sina ata lepe la usingizi.

Ulikosa usingizi wenyewe au ulikosa lepe lake??!!
 
Inaweza ikawa ndio sababu mkuu.Ukosefu wa nguvu za kiume umekuwa jangs la kitaifa ckuiz.
 
Back
Top Bottom