Unapoenda kufungua akaunti ya Akiba, na kutarajia kupata faida ya asilimia tatu kwa mwezi, hapo hujapanda mbegu? Benki nazo ni sawa na DECI, lakini hazisemi kwamba wanafanya wanayoyafanya DECI? Tatizo ni kwamba, wanataka sisi tupate kidogo wao wachukue kikubwa. Mfano, ukichukua mkopo (kama UKIFANIKIWA.... maana kuchukua na kufanikiwa ni mambo mawili tofauti....) wa Shs. 10 milioni, utarejesha Shs. 16 milioni ndani ya miaka 5, hii ni kwa CRDB. Lakini ukiwekeza Fixed Deposit Account ya Shs. 1 milioni, utavuna Shs. 3 milioni baada ya muda huo huo wa miaka 5. Kupanda "mbegu" huko CRDB unavuna Shs. 50,000 kwa mwezi, lakini wakichukua "mbegu" yao na kukupa wewe, unawarejeshea Shs. 100,000 kwa mwezi. Sasa kwa nini wamiliki wa CRDB na wezi wengine wasiende kupanda mbegu Keko? Jibu unalo! Tatizo sisi Watanzania ni vichwa maji. Kila jambo geni tunalipiga vita, tukiambiwa hiki kibaya, hatuulizi ubaya wake ni upi, tunasema: SAWA! Tutakuwa kondoo mpaka lini? Kwa nini tunakubali kila tunachoambiwa? Haya, wanachama wa DECI wamekatazwa kukutana na kujadili hatma ya fedha zao, mahali popote pale, kwa amri ya Kamanda Kova. Sawa? Jiulize... Kova anatoa amri kwa minajili gani? Anatumia kifungu gani cha Sheria? Haki ya Kukutana (Right of Peaceful Assembly) imeainishwa wazi kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sasa toka lini utaratibu wa watu kulazimika kuomba KIBALI kwa Polisi (mbwa wa mafisadi... samahani, mtaniwia radhi, lakini huo ndio ukweli!) ulianza, mimi sijui. Na Watanzania walivyo na nidhamu ya woga, basi, watakubali tu! Serikali imefunga akaunti za DECI, ili iweje? Hizo pesa za Watanzania watazipataje, iwapo akaunti zimefungwa? DECI watarudishaje hizo pesa kwa wanachama wao? Tutakuwa WAOGA mpaka lini? Tutakuwa WAJINGA mpaka lini? Tuamkeni, tufungue macho, TUMEINGIZWA MJINI! WIZI MTUPU! ./Mwana wa Haki! Na bado nitasema! Siogopi kufa! Siogopi kutishwa! Kufa ni WAJIBU wa kila mwanadam!