Nadhani wao wenyewe wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kudharauliwa.Naweza kusema wenyewe wanajidharau na wanatoa mwanya wa kudharauliwa.Inatakiwa tufike mahali tuondokewe na haya mawazo tegemezi ya kusubiri mshahara wakati unajua hautoshi kabisa.Na siku zote ujue Pesa inamchango mkubwa wa mtu kuheshimiwa au kudharauliwa.Waache kufanya mambo ya kujidharaulisha.Matatizo walito nayo yawape changamoto ya kujikwamua kiuchumi.Zipo kazi nyingi za kufanya na kuwaongezea kipato bila kuharibu utendaji wao.Ukiisubiri serikali ikuangalie utaishia kulia kila siku mapaka Yesu anarudi.