Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Kuna vitu vya ajabu hili nalo ni la ajabu, kuna wafanyabiashara wanafanya biashara kwa kuzitangaza mitandaoni ila wanazima simu, au unakuta wengine hawapokei simu au hawajibu meseji au kusoma jumbe za mitandaoni na kuzijibu ikiwemo maswali hii ni ajabu kabisa.
Hivi hawa wanakuwa hawajui wajibu wao au wanajaribu biashara? Maana unapoamua kufanya biashara kwa njia ya mtandao simu unatakiwa kuwa nayo karibu maana ndio kama injini ya biashara ya kukupatia wateja wako sasa wewe unaweka simu sijui chumbani unaenda kukaa nje nani apokee hiyo simu?
Hebu badilikeni muende sawa na matangazo yenu, unakuta mtu kapost karibu viatu na picha kama zote, bei hajaweka mara oo njoo inbox, nije inbox kufanya nini na ungeweza kuweka kila kitu wazi tukamalizana hapo, au hujaweka mahali pa duka lilipo wala mkoa na meseji za wanaouliza maswali kama bei gani hajibu pia mnakera sana na kufukuza wateja wanaojitambua.
Badilikeni bwana, mnakera mjue mnakera sana.