Kwa nini Wakenya wameanza kumpigia debe January Makamba kuwa Mwenyekiti wa Tume ya AU

Kwa nini Wakenya wameanza kumpigia debe January Makamba kuwa Mwenyekiti wa Tume ya AU

Ikaria

Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
93
Reaction score
238
Raia wengi wa Kenya katika mitandao ya kijamii hasa ule wa X wameonekana 'kumgeuka' mgombea wao wa nyumbani Raila Odinga na badala yake sasa wanamuunga mkono January Makamba kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika(AU).

Katika taarifa inayosambaa mitandaoni, Wakenya wanadai kuwa wamuzi wao umetokana na kugundua ya kuwa mgombea wao Raila Odinga anatumika kisiasa na watu kutoka nje ya Bara la Afrika.

Hili linakuja saa chache tu baada ya Raila Odinga kuonekana kusimama na upande wa Serikali kwa kutupilia mbali wito wa vijana wa kumtaka Rais William Ruto kujiuzulu.

Kiongozi huyo wa upinzani alikosoa shinikizo la waandamanaji wanaomtaka Rais Ruto ajiuzulu akieleza kuwa hatua hiyo haitakuwa na mabadiliko yoyote katika Serikali kwani Naibu wa Rais Rigathi Gachagua ataishia kutekeleza sera zilezile zinazopigiwa kelele.

Kauli hii ya Odinga sasa imetafsiriwa na wengi kuwa ya usaliti na wengi kumtaja kama kiongozi asiyekuwa mwadilifu; jambo ambalo limepelekea Wakenya wengi kumpigia debe January Makamba, wakimtaja kama kiongozi mwadilifu.

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika anatarajiwa kutokea katika Ukanda wa Afrika Mashariki, na tayari Kenya ilikuwa imeanza mchakato wa kufanya kampeni kurai mataifa ya Afrika kumchagua Raila Odinga.

Ikumbukwe Tanzania bado haijajitokeza rasmi kumuunga mgombea yeyote mkono na Wala haijamtaja Makamba kama mgombea wake.

20240718_165851.jpg
Screenshot_20240718-170226.png
Screenshot_20240718-170012.png
Screenshot_20240718-165946.png
Screenshot_20240718-165938.png
Screenshot_20240718-165928.png
Screenshot_20240718-165914.png
 
Kuna wakati na muda ndg zangu hasa sisi tulio hapa JF tuwe makini sana.

Pesa ina nguvu sana, hapo inaweza kuwa kuna watu wamepenyezewa umande ili kuwarubuni watz as kinachotokea kwa yule mzee Magoma na Yanga.

Yaani inatakiwa umakini mkubwa sana kunapoibuka ajenda zisizoeleweka katika kipindi hiki tunapokaribia uchaguzi.
 
Raila hajasaliti Gen Z

Vijana wengi waongozaji maandamano ni vijana wa Laila

Makamba ameanzisha Uzi kupima watu
 
Back
Top Bottom