Mzee wa Rula
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 8,169
- 3,351
Kuna kitu huwa kinanishangaza sana toka kwa wanaume, yaani inapotokea mwanaume ana uhusiano wa kimapenzi na msichana basi tulio wengi hujiona kama ndiyo tunanafaidi sana na kupelekea kujisifu wazi wazi. Hii ya kujisifu kuwa fulani labda ni demu wangu inaweza isiwe kero , kero yenyewe ni pale mtu anaposijifu jinsi alivyofanya mapenzi na huyo mtu wake na kujikuta anatoa siri za chumbani ambapo hazijafuata mkondo sahihi kutoka. Mkondo ninauokusudia ni kama vile, kuomba ushauri, kusuluhisha ambapo katika kutafuta ushauri au kusuluhisha baadhi ya siri za wapenzi hujikuta zimetoka. Hili limejithibitisha sana kwa vijana ambao bado hawajaoa na wanaume wengi wenye ndoa lakini wana nyumba ndogo.
Swali langu kwa nini wanaume tunakuwa tunajisifu sana kama vile wanawake hawafaidi kabisa katika mchakato wote wa mapenzi? Sababu ni nini hasa?
Nawasilisha kwa mabingwa wa saikolojia na mahusiano waniweke vizuri.