nadhani kuna sababu nyingi, baadhi ni:-
1. tamaa shoga, haswa pale anaposimuliwa mambo ya yule mwanaume lets say unamwambia shoga yako "bwana wangu mjuzi ananipeleka ananifanya hivi au vile" au pale shosti anapoona bwana wa mwenzie anamjali anampa hiki au kile simu mara kwa mara; anadhani akiingia na yeye atapata, au kama mwanaume ana fedha shosti anaweza kumtokea akijua atapata fedha nk
2. tabia mbaya ya mwanaume; kuna mijanaume mizinzi inatongoza hadi ndugu zako wa damu sembuse rafiki. na ukikuta na shosti ana tabia mbaya ndo inakua balaa
3. baadhi ya mashosti wanafanya hivyo kukomoa "tuone anachoringia kwa huyo mwanaume wake" au " naweza kumchukua huyo mwanaume wakati wowote"
4. wengine labda wana matatizo kisaikolojia jamani, kuna mdada yeye ni kujirahisi kwa waume wa wenzie, akimpata anafanya kama competition fulani, akiweza kupata attention ya mume wa mwenzie ndo anapata faraja. Sijui huu ni ugonjwa au vipi, ilifikia kipindi wanawake walipomshtukia wakawa wanamkwepa
wanawake wanatakiwa kuwa makini sana na hawa mashosti, usiache rafiki kumzoea mumeo/boyfriend. lazima kuwe na limit ya uhusianao kati ya rafiki na mume/boyfriend. haiwezekani kila rafiki akawa na namba ya simu ya mumeo, na ampigie anavyojisikia. akitaka kitu kwako badala ya kukupigia wewe yeye anampigia mumeo. Hili pia linaenda hata kwa wanaume, asimzoee sana shemeji yake.
pia mwanaume makini aliyependa kwa dhati, anayemuheshimu mwenza wake hawezi kutembea na shosti wa bibi yake, kama kutoka atacheza mbali