Kwa nini wanawake wanapenda sana kutikisa kiberiti?

demokrasia

Member
Joined
Apr 6, 2011
Posts
52
Reaction score
5
Mimi ni mwanaume nina mpenzi wangu ambaye anapenda sana kutishia kuniacha kila inapotokea ugomvi kidogo tu. Mara nyingi nimekuwa nikijitahidi sana kuomba msamaha hata kama kosa ni la kwake, ili tu mambo yaishe tusonge mbele. Wiki moja iliyopita kama kawaida yake amenitishia kuniacha na akaniambia kuwa hanipendi, hivyo niache kumpigia simu ili nimsahau. Lakini safari hii sijataka tena kuomba msamaha, badala yake nimemwambia kuwa ok waweza kwenda, nitapata mpenzi mwingine. Zikapita siku nne sijamtafuta, ghafla yeye kaanza kunitafuta na kuniomba nimsamehe kwa maneno aliyoniambia. Wana JF naombeni mawazo yenu, hii maana yake ni nini?
 
huyo siyo, umepotea huko, achana naye mtaishia pabaya, tafuta wa kufanana naye, mambo ya kutikisha kiberiti sijui kutishia kuvunja yai yalishapitwa na wakati
 
Nimependa saana response yako ya mwisho ya kuonesha msimamo na kwamba you don't care any more... IMO kama unampenda na unaona kabisa anakufaa ni heri umrudie maana kisha tia adabu kua you have limits too za kua pushed... Na kabla huajafanya hivo mueleze ukweli wako wa jinsi anavokuboa na kwamba abadilike....
 
pole sana demokrasia,mi naona mpe mda labda mpo wengi na anashindwa kuamua yupi ana pendo la kweili.mweleze kuwa unampa muda ili a-reconcile na huhitaji vitisho in future.
 
Usipende kuish maisha ya tamthilia. Uwe mkweli. Mpenz wako ni vyema akajua kitugani unakipenda na kitugani hupendi. Anapo fanya makosa mweleze. Utageuka mume ***** halavu wenzako watakula mzigo kilaini. BE A REAL MAN!
 
hii tabia ya kurudia rudia slet naomba invisible umpe BAN huyu kijana ili akome
 
Usipende kuish maisha ya tamthilia. Uwe mkweli. Mpenz wako ni vyema akajua kitugani unakipenda na kitugani hupendi. Anapo fanya makosa mweleze. Utageuka mume ***** halavu wenzako watakula mzigo kilaini. BE A REAL MAN!

Asante mkuu.
 
Pole mwenzangu nadhani tulikuwa sote katika tatizo moja mimi nami ni mara sita zinafika Mrs ana niambia amechoka na anataka aondoke mwisho uzalendo ukanishinda nikamruhusu. lakini karudi na hasemi kitu.
 
KUwa mweli kwake na msiogopane bana
maisha ni kuishi bila kuw ana wasi wasi kila siku
Maisha gani ya kuwa wewe ndio wa kusugua goti uonekane mkosaji kila mara wakati mwingine ambao makosa sio yako
Kama anakupenda mwambie na yeye ajiweke katika viatu vyako wewe akae hapo ulipo aone ni nini kitatokea
 

Nashukuru sana mkuu. bila msimamo hawa watu wanasumbua sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…