Kwa nini wapinzani hawafungui kesi dhidi ya polisi?

Magobe T

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2008
Posts
5,602
Reaction score
3,845
1. Kuna madai kwamba mara nyingi wapinzani wanapokuwa wanataka kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kukusanyika au kuandamana kwa amani huwa wanazuiwa na wakiendelea na kukusanyika au kuandamana huwa wanapigwa na kudhalilishwa (kama ilivyotokea kwa Prof Ibrahim Lipumba) kwa madai kwamba hawakutii amri halali ya polisi ya kuzuia maandamano au mikusanyiko, ambayo huwa polisi wanadai kuna taarifa za kiintelejensia za uwezekano wa kutokea uvunjifu wa amani.

2. Hali hii imekuwa ikijitokeza mara kwa mara na baadhi ya viongozi na wafuasi wa vyama hivyo wamekuwa wakifunguliwa kesi za jinai mahakamani.

3. Je, kwa vile kesi nyingi za namna hii huwa mahakama inawapa ushindi wapinzani, hawawezi kufungua kesi dhidi ya jeshi la polisi kuomba fidia kwa udhalilishaji, kuwapiga na matumizi mabaya ya ofisi kinyume na sheria za nchi?

4. Tafadhali, naomba nieleweshwe sheria zinasemaje kwa hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…