Mtangoo
JF-Expert Member
- Oct 25, 2012
- 6,167
- 5,613
I hope Mods hawataunganisha na Nyingine maana hapa ninataka kuonyesha hakuna Mantiki ya kuendelea na Muungano, hasa baada ya Ujio wa rasimu yetu.
Ukiipitia rasimu yetu utagundua ina "impossibilities" nyingi sana. Nitazijadili chache ambazo zinanipelekea kwenye hitimisho kuwa tunapaswa kuwa na serikali mbili tu, yaani Tanganyika na Zanzibar.
Moja, ardhi sio suala la Muungano na hivyo rais wa Muungano hatakuwa na ardhi aliyo na mamlaka nayo. Mamlaka ya ardhi kwa maana hiyo itakuwa kwa serikali hizi mbili. Swali ni kuwa, Je rais wa Muungano atatoa wapi mamlaka kama hata ardhi hamiliki? Anawezaje kutoa order kwa rais wa Tanganyika ilhali rais wa Tanganyika ardhi ni yake? Je tunatengeneza mfano wa Vatican ndani ya Italia?
Hata suala la sheria ya ardhi itakuwaje? Kama Zanzibar na Tanganyika wakisema hakuna raia kutoka nchi nyingine kumiliki ardhi yetu, Nini faida ya kuwa na uraia wa Muungano?
Pili, Suala la Majeshi. Rasimu inasema nchi husika zaweza kuunda majeshi yao wakiamua kufanya hivyo. Sasa kama maraisi wa hizi nchi wakiamua kuunda "JWT" na "JWZ" what will be the use of JWTZ? Na Funding ya JWTZ itatoka wapi maana kama Tanganyika na Zanzibar watakuwa na majeshi yao, then hawataona umuhimu wa kulipa gharama za majeshi ya Muungano. Kwa maneno ya mzee wangu, "Litakuwa kama Jeshi la UN la kujitolea askari". Sasa kuna haja gani ya kuwa na JWTZ wakati nchi washirika wanaweza unda majeshi yao? Hili pia halina mantiki!
Tatu, Maliasili zote zitakuwa chini ya usimamizi wa serikali husika na hivyo serikali ya Muungano haitakuwa na chanzo chochote cha mapato amabacho ina sauti nacho. Kwa hiyo nahoji ni nani ataketoa fedha? Katiba inasema washirika wana haki sawa na kwa sababu hiyo (by implication) wana wajibu sawa katika serikali hii. Kusema Zanzibar itoe gharama sawa ni kuionea maana haitaweza na kusema Tanganyika ichangie zaidi ni kuionea pia kwa kuwa washirika wana haki sawa. Kwa hiyo hii ni "impossibility" nyingine!
Kufupisha mambo mareefu ni kuwa Muungano wa serikali tatu hauafai. Unaziongezea Tanganyika na Zanzibar mizigo isiyo na tija kabisa. Mambo ambayo serikali ya Muungano inatakiwa kuyafanya yatakuwa "effective" yakisimamiwa na serikali husika.
Solution inayobakia hapo ni aidha serikali moja au serikali mbili zenye mamlaka kamili. Serikali moja ni impossibility nyingine. Zanzibar wamekuwa na malalamiko yao kuwa Muungano unawaonea na majaribio kadhaa yamefanywa na Wazenj kuhakikisha wanatoka. Kwa hiyo kuwalazimisha si sahihi. Kama alivyosema mama yangu "Zanzibar wanaona wameonewa na Tanganyika wanaona wamewapendelea sana".
Kwa maana hii suluhisho ni kuachana kwa amani tuendelee na udugu kama Kenya, Rwanda, Burundi, Malawi n.k. Hii itakuwa njia bora zaidi kuliko tukiachana kwa staili ya Sudan au Ethiopia na Eritrea. Muungano ulikuwa ni mzuri na umeshamaliza lile ulipaswa kulifanya. Conditions zilizopelekea Muungano hazi apply tena leo kwa hiyo ni vema tukauweka pembeni. Bado kuna SADC, EAC na mashirikisho mengine, tukutane huko.
Wananchi hatuna haja ya kuogopa. Tuiambie serikali yetu tunachotaka bila vurugu wa rabsha. Tuseme kuwa Muungano inatosha na tuwe active maana nafasi hii ni yetu. Pili tuwe makini na wanasiasa wote bila kujali vyama vyao. Wao wana "interest" zao kama vyama na sisi tuwe na interest zetu zinazovuka mipaka ya vyama na vinavyotuunganisha kama taifa.
Ikitokea tukawa na katiba mbaya, watoto na wajukuu zetu wataumia na pengine hawatakuwa wa chama chako au hata kuwa na chama. Hebu tueke pembeni maslahi yanayotugawa na tuijenge nchi yetu tukianza na Katiba mpya na nchi mbili mpya!
Wasalaam!
- BH
61.-
- Kwa mujibu wa Katiba hii, Washirika wa Muungano ni Tanzania Bara na Zanzibar.
- Serikali ya Tanzania Bara itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Tanzania Bara.
- Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Zanzibar.
- Washirika wa Muungano watatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na Katiba zao.
- Washirika wa Muungano watakuwa na hadhi na haki sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano na watatekeleza majukumu yao kwa masuala yote yasiyo ya Muungano katika mamlaka ya Washirika wa Muungano kwa mujibu wa masharti yatakayowekwa na Katiba za Washirika wa Muungano.