Kwa nini watu wengi wanarejea kwenye dini za mababu (matambiko)?

Bongotunacheza

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2018
Posts
1,821
Reaction score
3,980
Ndugu zangu Tanzania hakuna tena Wakristo wala Waislamu. Nenda kwenye magroup mbalimbali mfano la Wachokonozi, group la yule. Jamaa wa Morogoro alie trend mwaka jana naagroup mengine ya dini kuna kuna idadi kuwa sana ya watu wenye majina yanayoitwa majina ya Kikristo na Kiislamu wakitetea imani ya Ibada za mababu (Matambiko) na kuponda dini hizi tulizo letewa (Ukristo na Uislamu).

Sasa hivi kibao kimegeuka. Zamani ilikuwa ukipenda Ukristo au Uislamu ndo unashukiwa vibaya mno lakini sasa hivi ole wako uponde habari za mabibi na mababu (Ibada za mizimu) utashukiwa vibaya mno.

Je nini sababu ya Watanzania kusifia ibada za mizimu hadharani tofauti na zamani?

1. Je ni kwa sababu zina nguvu sana na zina majibu ya papo kwa papo?

2. Watanzania wamechoshwa na uongo na utapeli wa mafundisho ya dini za kigeni?

3. Wamepata ujasiri wa kutoka hadharani (Walikuwa wana practice tangu zamani)
 
Kanisani tunaenda kwa ajili ya kuzikana, hamna zaidi ..... stori za kwenye Biblia zina walakini japo ndio afadhali ukilinganisha na Dini nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…