Kwa nini Yanga mumeamua kututesa mashabiki?


Nakufungwa kwa simba goli 2-0 na Yanga kunatabiri ushindi WA ccm October 25
 
Viongozi wetu wanakubalije timu itumiwe na wanasiasa?"Hawajui mashabiki wao ni wa vyama vyote?

Unazungumzia viongozi wa tim ipi kati ya hz
 

Attachments

  • 1443876842518.jpg
    9.9 KB · Views: 214
  • 1443876854897.jpg
    35.3 KB · Views: 202

Saga chupa unywe,hapa kazi tu
 
Ni kweli aisee wasikie kilio chetu yaani hata mm niko radhi kuichukia Yanga na hata nisiishabikie kwa kuwa imekaa ki ccm bana mnatukera sana
 
unaposhabikia ujinga na wewe unakuwa mjinga hapo kama nini hama tu shabikia timu nyengne kwanin uwe mjinga?
 
Yanga tuko imara, sisi kwetu ni kazi tu majungu peleka msimbazi
 
kawaida saaaana mtoa post furaha ikizidi hakuna wa kuizuia ndio mpira huo mm nilieanza kuishabikia Yanga miaka ya 80s nimeona vituko vingi vizito kuliko hv.
 
Nazungumzia wale waliobandika bango la magufuli kwenye ofisi za Club. yaani yanga.

Mahusiano ya Yanga na CCM ni ya kihistoria, yamechanganyika mithili ya sukari na chumvi ambapo chekecheo haliwezi kuyatenganisha labda zitumike mbinu za kikemikali kama vile crystallization, evaporation au hata paper chromatography!

Baada ya uhuru chama (TANU baadaye CCM) kiliunda jumuia za chama kama vile JUWATA, UWT, UVT na Umoja wa Wazazi hapakuundwa Jumuia ya michezo hivyo uko huru kuishabikia Yanga bila ya kuwa Mwana CCM na vivyo hivyo Mwana CCM halazimiki kuishabikia Yanga. Sasa wewe ni kitu gani linakukwaza? Kama hupendi CCM, andaa 'kichinjio' chako uwahi foleni hapo Oktoba 25.

Mpinzani mkuu wa Yanga ni Simba, nakuhakikishia ndani ya Simba kuna Wana CCM wa kumwaga vivyo hivyo ndani ya Yanga kuna Wapinzani wa kumwaga.

Aliyebandika bango la Magufuli pale klabuni ni Mwana Yanga ambaye pia ni Mwana CCM, huzuiliwi hata wewe Mwana Yanga ambaye ni Mpinzani kubandika picha ya Lowassa hapo klabuni, hizo ni kampeni za muda mfupi tu lakini Yanga itadumu milele. Baada ya Uchaguzi Mkuu atakayeshinda atakuwa ni Rais wa Watanzania wala si Wana Yanga au Wana CCM na Wapinzani.

Yanga Mbele Daima Nyuma Simba!
 

umenena vema mkuu
 

Uko huru kuwaza unavyotaka....ila SS ni ID yangu na sina ingine....unless kama unawashwa unahitaji nikukune. Niache nishangilie ushindi wa diwani na mbunge huku nikisubiri ngoyai mumtangaze uraisi.
 
Uko huru kuwaza unavyotaka....ila SS ni ID yangu na sina ingine....unless kama unawashwa unahitaji nikukune. Niache nishangilie ushindi wa diwani na mbunge huku nikisubiri ngoyai mumtangaze uraisi.

Uraisi ni wa Lowassa
Urais ni wa Magufuli

Hongereeni sana waheshimiwa.
 
Uraisi ni wa Lowassa
Urais ni wa Magufuli

Hongereeni sana waheshimiwa.

Kwa sasa nashangilia ushindi wa SAID KUBENEA na GODFREY CHIKANDAMWALI kama wabunge na na diwani wa CHADEMA respectively....im busy habari za kufundishana kiswahili fasaha kafundishe familia yako. BTW thanks kwa hongera yako na karibu lite za bariiiiiiiidiiii
 

Hongera siyo yako, ni maalum kwa ajili ya Lowassa na Magufuli ambao ni raisi na rais mtawalia, wewe hukutakiwa kuiitikia.
 

Ni mjinga tu huyo anashindwa kufahamu mgombe ubunge moshi mjini aliyeshindwa ni kiongozi ktk klabu ya yanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…