Lucas
JF-Expert Member
- Dec 3, 2011
- 2,457
- 1,110
Hello wakuu,
Leo nimeona blogs kadhaa zimeripoti kwamba mheshimiwa Jamal Malinzi amempa kocha mkuu wa taifa stars kazi ya kuiondoa Uganda kwenye michuano ya CHAN ili kulinda kibarua chake.
Kwanza kabisa nakiri kuwa mimi ni mshabiki zaidi wa Taifa stars kuliko timu yoyote ya mpira duniani, iwe ya klabu au ya taifa. sijawahi na sina mpango wa kununua jezi ya aina nyingine yoyote isipokuwa taifa stars, japo ni mshabiki wa Yanga, Chelsea na Madrid pia.
Nikiangalia matokeo ya tangu aje kocha huyu, hakika siwezi bet na mtu timu yangu ikicheza hata na timu ya daraja la nne leo hii. Tumefungwa na timu karibu zote za jirani zetu, timu ya 160 kwenye FIFA ranking leo yaweza tufunga!!
Nina hamu kubwa sana huyu kocha aondoke na kutokana na hilo najitolea kuwa mshabiki wa Uganda ili stars yangu niipendayo ifungwe ili Nooj aondoke!!
Nakaribisha wadau zaidi tuungane kuishangilia Uganda ili Nooj aondolewe kabisa. Maana kwa Lugha ya kawaida tumesema sana hadi bungeni imepelekwa lakini TFF hawasikii kabisaaaa.
Sasa naomba tuwakaribishe na wengine kuungana nasi (kwa watakaoona vyema) kuishangilia Uganda the cranes watufunge goli nyingi tuuu za kutosha ili Nooj aondolewe kabisaaa
source: MALINZI AMUAMBIA NOOIJ; "TUKITOLEWA NA UGANDA TU, FUNGASHA VIRAGO MWENYEWE" | BIN ZUBEIRY

Last edited by a moderator: