Passion hustler
New Member
- Sep 17, 2021
- 1
- 1
Kwanza kabisa, ninapenda kuihasa jamii kuhusu suala la kufanya kazi (kujishughulisha), ili iweze kuondokana na Uzembe na Umaskini. Pia Wazazi au walezi, wanapaswa kuwafunza vijana wao namna ya kuweza kuyakabili Maisha wakiwa Shule au hata nje ya shule, ili hata wanapohitimu wawe tayari wanajitambua na wala wasiwe ni vijana wanaojihusisha na maadili mabovu,
Ni lazima kwa kila Mfanyakazi au Mfanyabiashara kulipa kodi ili kuiwezesha Serikali katika kuleta Mabadiliko chanya hasa katika Nyanja za kiuchumi na Miundombinu. Na inabidi kila Mfanyakazi au Mfanyabiashara aweze kuwa na Malengo chanya, kwake yeye na kwa Jamii ili faida irejee kwa wote, Asasi za kiuchumi zinapaswa kutoa Mafunzo kwa Wananchi kuhusu Suala la kujikimu kimaisha kwa kujishughulisha na masuala kama ; Ujasiriamali na Uwekezaji, Na Kwa kila Mfanyakazi aliyeajiriwa aweze kuwa mtunzaji na mtumiaji mzuri wa pato lake ili kukwepa hasara itakayoweza kumtupa kwenye Umaskini, pia kujituma katika mwenendo mzuri wa kimaadili kwa mfano: kuwahi kuamka asubuhi na mapema na pia kuwaheshimu watu wa rika zote ili hata anapotaka kufanya jambo fulani kuhusu biashara ya aina yoyote ile, hiyo jamii iweze kumuunga mkono katika mambo yake atakayotaka kuyafanya.