Kwa pamoja tuwasaidie watia nia wetu kukubalika kwa wananchi

Kwa pamoja tuwasaidie watia nia wetu kukubalika kwa wananchi

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu ilikuwa ni muhimu sana kutambua kuwa ushindi utapatikana tokea katika mavuno ya haki ya kura za wananchi.

Ilikuwa muhimu zaidi hili kufahamika kwa wagombea wenyewe, wafuasi na hata mashabiki wao.

Kura hazilamishwi wala kupatikana kwa ghiliba, matusi, nk, labda kama mgombea kajipanga vilivyo kukataa matokeo au hata kuukwiba uchaguzi tu. Kistaarabu tunasema, wa hivyo si mshindani. Kwa hakika huyo hatufai.

Kwa vile lengo kuu ni kuvuna kura halali, kila mtia nia na hatimaye kila mgombea atapata kura kutegemeana na kiwango chake cha kukubalika kwa watu.

Je, mgombea anataka kukubalika? Ni vyema kuwasaidia wagombea wetu kuyafamu bayana ili wasije kuwa wamepoteza mguso kwa jamii.

Ninaamini mgombea huyu:

IMG_20200804_210728_515.jpg


Ni mpenzi wa Mungu kwani kwa hakika ametanguliza haki mbele. Haki itamfanya kukubalika vilivyo kwa watu. Nani asiyependa haki?

Kwanini sababu kama hizi zinazotuongoza kuliko haki ni msiba mkubwa kwa wagombea wengine na hali bado wanapenda kukubalika?

Tatizo la matakwa kama hayo takribani sita ya wajumbe na mahakimu wa watia nia "come Oct. 28," ni nini hasa?

Je, ni takwa lipi katika hayo ambalo mgombea awaye yote anakwazika mno nalo kiasi yu radhi kufa na tai shingoni? Je labda ni kwa nini?

Tuelimishane.
 
Nitaweza kuwasaidia wagombea wote lakini jiwe siwezi kumsadia hata ndotoni.
 
Vipi corona imeua wangapi kwenye familia au ukoo wako?
 
Nitaweza kuwasaidia wagombea wote lakini jiwe siwezi kumsadia hata ndotoni.

Nadhani tatizo si mtu bali pana mambo ambayo akiyafanya waungwana wanaweza badili msimamo. Mfano awe mwenye kulenga haki kama ilivyo orodheshwa kwenye mada.

Bado patakuwa na tatizo mkuu?
 
Nadhani tatizo si mtu bali pana mambo ambayo akiyafanya waungwana wanaweza badili msimamo. Mfano awe mwenye kulenga haki kama ilivyo orodheshwa mada.

Bado yatakuwa na tatizo mkuu?
aliyekuelewa anisadie kunifafanulia zaidi.
 
aliyekuelewa anisadie kunifafanulia zaidi.

Wapi hapaeleweki mkuu? Sote tunajenga na tuendelee kujenga nyumba moja.

Tuwasaidie wagombea wetu kujua nini tunataka.

Angalau pia watushawishi ni kwa nini wasitupe tunayotaka?

Ikumbukwe kuwa wao ni watumishi wetu watarajiwa wa kutenda tunayotaka sisi siyo wanayotaka wao.
 
Magufuli alipaswa afikishiwe habari iliyopo kwenye uzi kama huu.

Haipo namna nyingine ya kukubalika.kwa watu.
 
Back
Top Bottom