Taitzo la kipa ni dogo sana kwa simba. Niliandika mara nyingi sana kama mwezi mmoja uliopita hapa jamvini lakini nilishambuliwa sana na wadau.
tatizo la kubwa la simba lilianzia pale walipomtimua mayanja na kumuacha Omog halafu wakaja tena kumtimua Omog badala wamrudishe Mayanja kwa muda mpaka ligi iishe mwakani watafute kocha mwingine viongozi wakalikoroga tena wakamuachia timu djuma. timu inamiliki mpira sana (kwenye mechi karibu zote za mapinduzi ilimiliki mpira vizuri) lakini haina mbinu za kufunga na haina mtu wa kabadilisha matokeo muda wowote kama alivyo okwi
Tatizo kubwa la pili la simba ni kuwa hawana mshambuliaji wa kati atakayempa changamoto boko. Kabla ya dirisha dogo niliandika hapa kuwa simba ina mshambuliaji mmoja tu wa kati wa maana ambaye ni boko hivyo ilihitajika haraka sana watafute mshambuliaji analiyejua goli kwa kichwa, miguu yote miwili na hata sarakasi ili mradi purukushani mpira uingie ndaini badala yake wakaenda kuwekeza kwa kwasi na sasa wanavuna walichopanda. na nilisema hapa waongeze mshambuliaji mmoja wa ndani na mwingine wa nje. nilisema okwi ni winga, gyan ni winga (na imethibitika zanzibar), mavugo ni winga na luizio atolewe kwa mkopo arudishe kwanza kiwango chake kwani tangu aumie hajapata muda mrefu wa kucheza hayo yote yalipuuzwa.
Tatizo kubwa la tatu kwa simba nilisema ni fittnes ya wachezaji wanacheza vizuri dakika 60 tu baada ya hapo kila mtu anajua nini hutokea wanapokutana na timu zilizo na stamina, pumzi na kucheza kwa nguvu nikatoa mfano wa prison. hili pia limetokea kwenye FA cup walipotolewa na timu ya jeshi sijui ipo daraja la ngapi vile.
Kiujumla simba kuanzia golini, beki, katikati na hata winga ipo vizuri shida kubwa ni kocha djuma aondolewe arudishwe mayanja na kamati ya usajili ifutwe kwa sababu walipaswa kutafuta mtu wa kuwa anafunga tu wao wakaleta beki. Pia wachezaji wanaonekana hawana fighting spirit hapa ndio unaona umuhimu wa kuwa na kocha msaidizi matola au julio. kwenye mpira saa nyingine inahitajika kuhamasisha wachezaji wapambane wala sio ufundi ndio maana unaweza kuona timu ya hovyo inampiga barca au madrid.
Kwa mwenendo nina wasiwasi ubingwa tutausikia tena.