Rais Samia amekiri kusikia kelele na matusi ya watanzania juu ya sera zake na uongozi wake. Lakini amesema ameamua kujifanya kuwa kama "chura kiziwi" mpaka dhamira yake na lengo lake la litakapotimia.
Katika kauli yake hii nabaini mambo 2:-
1. Ni ule ugonjwa walionao viongozi wengi wa Afrika wa kudhani "cheo ni akili". Hivyo Samia kwa kuwa yeye ni Rais, basi anajiona yeye ndiyo mwenye akili kuliko watanzania wote. Ndiyo maana anapuuza maoni (yeye kayaita kelele) na ukosoaji (matusi) yao.
2. Watanzania wameporwa madaraka yao, hivyo Samia hayuko tena kwenye kiti cha urais ili kuwatumikia. Ndiyo maana kile wanachokitaka kinaitwa kelele na matusi. Kama Rais angekuwa yuko pale kwa kuwatumikia wananchi, basi angefanya kwa kadri wanavyopendekeza.
Siyo mara ya kwanza kwa Samia kutoa kauli ya aina hii. Hata wakati wa sakata la kupinga DP World, alijitokeza na kusema atakaa kimya na kamwe hatojibu chochote. Mwisho wa siku akausaini mkataba wa DP World uliokataliwa na watanzania.
Pia, soma=> Rais Samia: Wananitukana ili niwajibu, najigeuza chura siwajibu