Pre GE2025 Kwa Rais Samia kujifanya "Chura kiziwi" ni dharau kwa watanzania. Kwani yupo Ikulu kwa maslahi ya akina nani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Na pia wapinzani wadhibiti sana vitambulisho vya kupogia kura kwa sababu vitanunuliwa kwa bei kubwa sana .
Hawa namaa wana pesa nyingi sana walizojikusanyia kutoka kwa waarabu na madili ya kisanii kama ya sukari na mengine .
Ishu sio pesa kwa watawala wa CCM . Kwao ishu ni kurudi madarakani na kuendelea kuchota pesa mana hii nichi ni wazi kuwa ina pesa nyingi sana ,tatizo ni mifumo ya kudhibiti uporevu wa mapato . Huko kwenye hifadhi na mapori na mito na bahari kuna matrilioni ya pesa yanapotea kila siku. Watu wanajichotea wanavyotaka. Watalii wanaingia wengi sana na mahoteli yanavuna pesa nyingi sana huku serikali ikiambulia kiduchu kutokana na uswahiba kati ya watawala na wawekezaji. Wananyama na madini na gesi pesa za bure zinamwagika lakini zinaishia kwenye mikono ya wahalifu wa nchi na wanapanga kununua vitambulisho vya mpiga kura .
Nini kinatakiwa kufanyika:-
Wapinzani hasa Chadema wanatakiwa wahakikishe kuwa wanachama wao wanatoa nakala au kopi ya smart card ya vitambulisho vyao huko vijijini na hata mijini mana wajumbe wengi wa CCM ni vilaza hawataweza kutambua original na kopi.
Kisha vile original waviweke tayari kwa alili ya kumtoa mtu pale magogoni mwakani ikiwemo ni pamoja na wabunge wake walioshiriki kuharibu Taifa hili kwa wizi na rushwa.
Wajumbe wa CCM wakipita kununua vitambulisho vya kura basi wawape zile nakala ambazo zitakua zinafanana na original. Hii biashara itakua na faida kwa wauzaji lakini kwa wanunuaji itakua biashara kichaa.
CCM mwaka huu wakitoa pesa chukueni lakini Kura ni siri.

Watu wanaonunua kura ni wabaya kuliko Machangudoa .

Viongozi wa dini zote kama kweli mnamtumikia Mungu na kuhubiri kuwa Mungu yupo na ndiye Muumbaji wa vitu vyote iliwemo Nchi na rasilmali zake na sio CCM na watawala wake basi wasimame kidete kupinga Wizi wa kura na udhalimu wowote unaopelekea taifa kupata vipngozi madhalimu na wezi wasiojali hata uumbaji wa MUNGU na haki.
Asantee sana🙏
 
Nyerere hakuwa kiongozi wa viwango vya kupigiwa mfano. Alikuwa moja ya madikteta wabaya sana. Ni vile tu alitawala enzi za giza.

Kwahiyo siyo kila alichofanya Nyerere kinafaa kutumika kama rejea.
Hawa vyura viziwi usiwalinganishe na Nyerere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…