Uchaguzi 2020 Kwa rhetoric kama hizi, uwezekano wa jina lake kutokuwepo kwenye ballot paper unazidi kuongezeka

Uchaguzi 2020 Kwa rhetoric kama hizi, uwezekano wa jina lake kutokuwepo kwenye ballot paper unazidi kuongezeka

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Ni kama vile upinzani baina Tundu Lissu na Rais Magufuli ni personal.

Lissu anatumia lugha kali sana akiwa anamzungumzia Magufuli. Kabakiza tu kumtukana matusi ya nguoni hadharani [si ajabu faraghani huwa anamtukana hayo matusi ya nguoni].

Kwenye video hii kutoka jana akiwa Arusha, kuanzia dakika ya 1:29....baadhi ya watu kwenye umati aliokuwa akiuhutubia, walisikika wakisema ‘wewe ni ngosha bana’.

Naye aliposikia hivyo akajibu kwa kusema ‘eh mi sio ngosha....mi sio jiwe’.

Hakika, kwa kauli kama hizo, akiwekewa figisu ili hatimaye jina lake lisikuwepo kwenye ballot paper mwezi Oktoba, sitoshangaa kabisa.

Lissu wakati mwingine mdomo wake huwa hauna chujio kabisa.

Yani we siku hizi ni snitch acha wafanye siasa wenyewe huko, mwingine hapo ana uchungu wa kujua kwamba aliemsababishia kupigwa lisasi ni jpm,
Jpm nae anaona Lissu amebezi sana kwa hao mbuzi dume,
Sasa chuki miongoni mwao ni kubwa mno,

Na Jpm anaamini yeye ni bora hakuna kama yeye ilihali Lissu anaona kama ni mtu asie na maana mvunja sheria, mkandamizaji na dikteta.
 
Hata kama ningekuwa Mimi ningetoa lugha kali kila nikiongea kama ulinipiga risasi 38 nikapona iweje nikuchekee hakuna cha kulemba Tena Lissu bado hajaongea mambo mazito Kuna mambo mengi bado yanatakiwa yakemewe Sana ya kupumbavu kwenye utawala wa Magufuli.

Kama anatukana wenzake anaogopa nini kutukanwa yeye yeye ni Nani hasa asisemwe huwezi kuwa Rais ukafikiria ni lelemama tu hata Kama unafanya maovu..

Lazima watu wakuchambue watakavyo.
 
Unakumbuka alipigwa risasi 16 .

Still anasavaivu

Hakuna awamu mpinzani alipigwa risasi huku nyuma .

Wazi wazi ndani ya makazi rasmi ya serikali na yenye CCTV

na waliompiga hawajakamatwa Hadi leo

Naomba nikukumbushe .

Ana mandate ya kuongea chochote maana anamjua adui yake .

Wewe endelea kuimba pambio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wee jamaa basi nikajua katukana tena nikajiuliza atukane wapi wakati majemedari muda wote tupo naye? Kumbe ni neno Jiwe...Si alijiita mwenyewe! Kuna mtu alimbatiza? Na kama akiitwa Jiwe anafurahia utajuaje?
"MIMI NI JIWE KWERIKWERI" Nimemnukuu na inawezekana ulikuwa humfuatilii
 
Alishamtukana mbona wakati anahojiwa na redio ya kenya wiki iliyopita..alisema kuanzia nyerere, mwinyi, mkapa na jk hawakujenga uwanja kwao sio hawa viongozi wa hivyo hovyo.
 
Alishamtukana mbona wakati anahojiwa na redio ya kenya wiki iliyopita..alisema kuanzia nyerere, mwinyi, mkapa na jk hawakujenga uwanja kwao sio hawa viongozi wa hivyo hovyo.
Kwahiyo hayo ni matusi?
Kuwa kiongozi wa "Hovyo hovyo" ni pamoja na kufanya vitu bila mipango madhubuti mfano kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa sehemu ambayo hauhitajiki hata kidogo, yani hakuna maana yoyote ya huo uwanja wa kimataifa kuwepo hapo!
 
Unajua kuwa ethiopian airlines ilipata shida ikatua kisongo airport arusha na kuhatarisha usalama wa watu sababu uwanja ulikuwa mdogo?
 
Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na viwanja vingi kuruhusu ndege kutua yanapotokea majanga au dharura kwa ajili ya usalama.

Lakini ni kwa sababu we upeo wako wa kuona mbali ni mdogo..kule kuna mbuga ya wanyama pia. Lakini ikitokea tatizo lolote mwanza airport, chato aitpory itatumika pia. Kwa hiyo ondoa huo ukungu
 
Hapo wala sijaona ukali wa kauli za Lissu. Nilichoona ni ukali wa hatua zilizochukuliwa dhidi ya Lissu, na serikali ya Magufuli :

1) Kuzuia bunge kumgharimia matibabu. Waziri wa Afya kuna wakati alitamka kwamba serikali iko tayari kugharimia matibabu ya Lissu, popote duniani, ali mradi ndugu zake wapeleke maombi. Hayo yalifanyika lakini serikali ikabadili msimamo. Ilionekana wazi hiyo ni amri ya Magufuli mwenyewe.

2) Serikali kuamuru Polisi wasimamishe uchunguzi dhidi ya tukio la kushambuliwa Lissu. Kwa kawaida Polisi hufungua jalada la uchunguzi na watu mbalimbali huhojiwa. Mfano majirani walioshuhudia tukio. Hapa tunaona polisi wamekataa kuanza uchunguzi, mpaka kwanza wamhoji Lissu mwenyewe na dereva wake. Kwa kauli za Polisi, na hasa IGP, inaonekana kwamba Lissu mwenyewe ndio mtuhumiwa namba moja.

3) Kufuta ubunge wa Lissu katika mazingira yenye utata.

Kwa sababu hizo kuu na zingine nyingi, serikali ya Magufuli inaonekana kumtarget Lissu kama adui na inamshambulia personally, with fatal consequences. Lissu is yet to return fire
 
Wee jamaa basi nikajua katukana tena nikajiuliza atukane wapi wakati majemedari muda wote tupo naye? Kumbe ni neno Jiwe...Si alijiita mwenyewe! Kuna mtu alimbatiza? Na kama akiitwa Jiwe anafurahia utajuaje?
"MIMI NI JIWE KWERIKWERI" Nimemnukuu na inawezekana ulikuwa humfuatilii
Nimekwambia acha kujipendekeza pendekeza kwangu. Mbona huelewi?
 
Back
Top Bottom