Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,015
- 2,493
Katika mchezo wa siasa unahitaji kuwa na akili nyingi sana kushinda "game". Lakini akili ya kwanza ni kumsoma, kumfahamu, kumwelewa aliyeketi kwenye kiti cha "executive" anawaza nini, nini hulka yake, ana uwezo gani wa kuona masafa marefu na tabia yake ikoje na ana uwezo gani wa kuadhibu au kusamehe jambo hata kama jambo hilo linaweza si tu kuangamiza Taifa lakini pia kumuangamiza yeye binafsi.
Katika utawala wa Rais John Pombe Magufuli (JPM) wateule wake walifanikiwa sana katika akili hiyo ya kwanza na kwa mantiki hiyo waliambizana na kukubaliana ni nyimbo zipi, mapambio yepi na kauli zipi zilimfurahisha "Mfalme" nao wakamwimbia, wakampambia na kumpa kauli zilizomfurahisha hata kama nyimbo hizo, mapambio hayo na kauli hizo ziliangamiza Taifa. Kazi ya wapambe (chawa) ni kuhakikisha wanapata mkate wao hata kama mwisho wa yote Mfalme atazama.
Kwa akili hiyo, wapambe wa JPM walijikuta wakisomba utajiri wa nchi hii kwa ubabe (si umame) bila hofu ya kuhojiwa. Waliomwabudu Magufuli kwa kicho wameshiba, wamenona kwa namna akaunti zao zilivyojaa noti hata za bandia na damu! Ama kweli, "kila zamu na kitabu chake" alijisemea Mzee Alli Hassan Mwinyi!
Alipoingia madarakani Mama Samia Suluhu Hassan "chawa" wake wakatumia akili ile ile ya kwanza. Wakati Samia Suluhu Hassan akiimba "Kazi Iendelee" wao kwa siri na usadi mkubwa wanaimba, "It's Our Time to Eat" (IOTE) kwa gharama ya wananchi wasakatonge na wadunda kazi. Genge lililoingia na Mama Samia wanawazomea "machawa" wa JPM na sasa wanashindana nani ana pesa nyingi katika akaunti ndani na nje ya nchi.
Mbinu waliyotumia na kufaulu kwa haraka ndani ya siku 720 tu ni kuwaimbisha Watanzania dhana ya Sukuma Gang ili waaminike kumbe ni wimbo sahaulishi ili waibe, wakwapue na kula bila hata kunawa! Hii ni aibu si kwa Taifa balj hata kwa wahisani walioamini kuwa utawala wa Samia Suluhu Hassan ungepambana na rushwa na ufisadi badala yake anaandika historia ya kukubuhu kwa ufisadi kuliko tawala ZOTE zilizotangulia kama kweli CAG Charles Kichere hakusema uongo.
Mabilioni (madudu) yaliyoibuliwa na CAG imeithibitishia Dunia na walimwengu kuwa Samia hana dhamira ya kweli kupambana na ufisadi, hawezi kupambana na ufisadi na mafisadi au naye ni sehemu ya mafisadi. Kwa maana kwamba mafisadi wamemteka nyara kwa kujua au bila kujua.
Kwamba tulipoimba Sukuma Gang wanafanya hiki na kile ililenga kumpumbaza Rais Samia Suluhu Hassan asijue wizi na unyang'anyi wa fedha za umma ulivyokuwa ukisukwa na kufanikishwa! Na katika kulifahamu hili, nani aliamini mkwara aliowachimba wateule wake kuhusu fedha za UVIKO-19 angetoke mwamba asiyeogopa rangi yake wala macho yake kukwapua fedha hizo? Kwani ukinitukana "stupid" hadharani napungukiwa nini ilhali mzigo ninao nakula na kunywa kwa raha zangu na mke/mume wangu?
Samia anaposema, "kula kwa urefu wa kamba yako" wao wanasema, "goli liko wazi ushindwe tu kufunga" huku wananchi masikini hawana hakika walau wa mlo mmoja kwa siku. Wapiga dili wana akili sana! Wamefanikiwa kupasuka nchi vipande viwili: matajiri kupindukia na masikini kupindukia. Tabaka la kati limefutika. Balaa linanyemelea Taifa soon!
Ni wakati wa kila mwananchi kuamka na kukataa aina hii ya uongozi wa kuwaonea haya na huruma mafisadi. Kila mtu aandamane chumbani kwake walau hata kila siku mara moja kumsema vibaya SSH. Mungu ana tabia ya kusikia na kufanyia kazi sauti ya mnyonge mmoja. Hata wasiosoma JF waambiwe kwamba kwa Ripoti hii ya CAG mwaka huu, Sukuma Gang wameibuka kidedea! Wajue kwamba Samia amezungukwa na wezi wenye akili kuliko waliomzunguka Dikteta Magufuli.
Naililia nchi yangu Tanzania!