Kwa uelewa wangu, nyakati ni kama vile Asubuhi, Mchana, Jioni, mwezi hata mwaka. Hapa unazungumzia nyakati. Lakini linapokuja suala la muda (yaani saa za wakati) ni sahihi kabisa kusema Kwa saa za Afrika mashariki. Hapa unakuwa unalenga saa za maeneo fulani tu,kwani muda umegawanyika katika kanda mbalimbali zinazotambulika kimataifa.Kwa mfano tunatambua kwamba Afrika mashariki (TZ,KN, na UG) ziko +3:00 (GMT au UTC) yaan ziko masaa matatu mbele kutoka mstari wa Greenwich au Universal Time Coordinated (UTC)(rejea jiografia yako ya sekondari).
Hivyo basi, saa mbili kamili za afrika mashariki maana yake ni kwamba, Kenya, Uganda na Tanzania ni muda uleule, lakini kwa saa bili hiyo ya Tanzania Uingereza itakuwa saa 11 jioni.
Kwa hiyo ni sawa kabisa