Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Ni siku nyingine tena tunakutana kujadìli changamoto zinazotukabili kama taifa. Jambo hili linahitaji akili zilizopevuta kutafakari na kujua ni nini sisi kama taifa tunahitaji ili tusonge mbele.
Kwasababu bila ya kuwa na akili zilizopevuka na zenye busara katika uongozi wa nchi yetu, maendeleo yetu itakuwa ni vigumu kuyafikia. Kwahiyo hili ni jambo la msingi sana. Kupevuka kwa viongozi wetu ni jambo la msingi.
Kupevuka kwa akili ni uwezo wa ubongo kuchanganua yaliyo sahihi kwa taifa letu na kuyafuata kwa faida ya umma. Jambo hili halipatikani hivi hivi, linapatikana kwa juhudi za kutaka kufanya yaliyo sahihi kwa juhudi katika kufikiri na kuchanganua mambo na kwa kudhibiti tamaa ili kuongoza mawazo na akili katika mkondo unaofaa.
Kwahiyo viongozi wetu lazima wawe wenye nidhamu ya hali ya juu kwasababu huwezi kuongoza watu kama wewe mwenyewe huwezi kujiongoza. Hili jambo ni muhimu .
Tunapoelekea kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. Naomba watanzania wajue kitu kimoja; baadae yetu kama taifa itategemea sana aina ya viongozi tutakao wachagua kwahiyo ni muhimu sana kuzingatia hili, ukombozi wetu utategemea sana kwanza ; aina ya watu watakaojitokeza kuomba kuchaguliwa kushika hatamu ya uongozi wa nchi yetu, lakini pili itategemea sana uwezo wetu wa kufikiri, kuchambua na kisha kuchagua viongozi watakao tuongoza kwa kipindi kingine kijacho.
Hili ni jambo muhimu sana tunapoenda katika uchaguzi tunaenda kufanya maamuzi yatakayoamua baadae yetu itakuwaje. Kwahiyo vijana wote na wazee na watu wenye familia ni lazima wawe makini na hili na walipe uzito unaostahili.
Natambua kuna kukata tamaa kwa watu wetu kuhusu uongozi na mwelekeo wa taifa letu. Watu wanaenda kwenye kuchagua lakini hawana matumaini hawaamini kama maisha yao yatabadilika. Hii ni changamoto inayotukabili kama taifa. Tunahitaji kiongozi atakayeamsha matumaini kwa watu wetu kwamba kesho haitakuwa sawa na jana. Haya ni matumaini ambayo watu wote wanayahitaji. Kwamba kesho ina ahadi tele kwamba kuna baadae nzuri kwa watu wetu wote.
Tunahitaji kiongozi ambaye ataamsha hisia za uzalendo, atakaye hamasisha watu walipende taifa hili na kulijenga taifa hili. Tumaini hili lazima limee kwa kila mtanzania, kama tunaishi na kama tuko wamoja baadae yetu kama watanzania itakuwa yenye tija.
Changamoto zinazotukabili kwenye siasa za nchi yetu sio za kuzibeza tunatambua pasipo siasa hakuna maendeleo yeyote makubwa tutakayofikia. Siasa yetu itaamua baadae yetu itakuwaje. Siasa nzuri katika taifa letu itajenga jamii nzuri na kinyume chake.
Siasa yetu ya sasa haitatufanya tufikie malengo yetu kama taifa au kujenga taifa hili kuwa imara tunahitaji kubadilika.
Watu wanatoa tushwa kununua uongozi, ulaghai na fitna mambo haya hayatoi ahadi nzuri kwa baadae yetu kama taifa yanatugawanya. Tamaa ya madaraka na uchu wa uongozi si dalili nzuri kwa taifa letu.
Vijana wa taifa hili angalieni wenyewe na mpime; katika dunia hii ni nani atakupa pesa ili akutumikie? Ni nani mwenye nia nzuri atadanganya ili apate nafasi ya kutumikia umma? Ni nani mwenye nia njema atatia fitna ili apate kutumikia umma? Wakati umefika sasa wa kuongea ukweli bila kutetereka. Kwasababu ni ukweli pekee utakaopeleka taifa hili mbele.
Baadae yetu ina ahadi tele kama tutabadilika, kama tutabadili mtazamo wetu kuhusu utaifa kama tutatazamana kama watu wamoja ambao baadae yetu ni moja.
Changamoto zilizo mbele yetu kama taifa ni nyingi. Kama taifa tunahitaji kusonga mbele bila kumuacha hata mmoja wetu nyuma. Tunatatizo kubwa la ajira nchini kwetu. Vijana wetu wanaishi pasipo kuwa na kipato cha uhakika haya mambo yanahitaji kuangaliwa na kupatiwa suluhisho la haraka.
Tuna changamoto katika elimu yetu tunahitaji kuangalia upya elimu yetu na kuiunda ili iwe na manufaa ya kutosha kwa taifa letu. Kuwajenga watu wetu kuwa raia wema watakaotumikia taifa hili kwa kulipenda kwa moyo wao wote.
Bila kujenga watu wetu katika tabia zinazofaa nchi haitosonga mbele. Kwahiyo elimu yetu lazima ijenge tabia za watu wetu katika nidhamu, uwajibikaji , uzalendo na uaminifu.
Tunaona kwa sasa madhara ya ufisadi katika taifa letu watu wetu ni lazima wafunďishwe umuhimu wa kutumikia na umuhimu wa taasisi zetu katika maisha ya kila siku ya utaifa wetu.
Hakuna mtu atakayepinga madhara ya ufisadi katika kurudisha màendeleo yetu kama taifa. Tatizo hili chanzo chake ni ubinafsi.
Kwahiyo ni muhimu na ni lazima kuondoa ubinafsi katika mioyo ya watu wetu kwa kuanzisha program mahususi kwa watoto wanaokua. shuleni na kwenye tv, kuwajengea uzalendo, umoja na roho ya kutumikia taifa lao.
Matatizo haya yanawezekana kuondolewa au kupunguzwa kadiri ya uwezo wetu sio matatizo ambayo hayawezekaniki yako ndani ya uwezo wetu.
Kwahiyo ni muhimu kuondoa haya matatizo ya kijamii na elimu bora itachukua nafasi kubwa katika kuyapunguza kwa watu kufahamu wajibu wao kwa taifa, jamii na kwa familia zao.
Vitu hivi vitatu vimeunganishwa kwa pamoja ili taifa lifanye kazi vizuri lazima viwe active. Kwahiyo matatizo ya familia ni lazima yaguse macho ya serikali yeyote makini. Kwa hiyo ni lazima tuji organize kama tunataka maendeleo.
Order na harmony katika familia hupelekea order katika taifa. Sisi kama taifa na kama jamii ni lazima tuwe na malengo mamoja. Ili tuunde jamii inayofanya kazi sawasawa kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
Bado tuna matatizo ya maji na umeme ni changamoto nyingine ambazo tunahitaji kukabiliana nazo kwanza ili kufanya maisha ya watu wetu kuwa Comfortable lakini pili kuimarisha uchumi wetu kwa kupunguza gharama za nishati hizi ili kuongeza uzalishaji na kuhamasisha uwekezaji hasa wa watu wa ndani ambao kwa dhati kabisa tunastahili kuwapa nguvu hiyo.
Kwahiyo bado tunachangamoto nyingi sana katika sehemu mbalimbali ikiwemo pia na afya za wetu.
Tunahitaji kwa sasa kiongozi atakaye set direction ambayo wengine watafuata kwa vizazi vingi vijavyo. Hatuhitaji kiongozi mwepesi mwepesi kwa maana hiyo. Tunahitaji kiongozi anayetambua changamoto zinazotukabili kwa sasa kama taifa. Ni dhahiri tumekosa maono na dira kama taifa. Kila mtu yuko na njia yake. Hii ni aina ya kiongozi tunayemtaka atakaye inspire watu wetu na kutengeneza dira.
Dira hii haipo tunahitaji kuijenga hatuna dira kama taifa. Mawazo yetu kama taifa hayako katika mkondo mmoja tunahitaji kujenga hii kitu. Tunahitaji kujenga watu watakaotumikia taifa hili katika misingi ya wajibu tatu ambazo zimeungana kwa pamoja;
Wajibu wa mtu kwa familia yake ukiungana na wajibu kwa jamii yake na kwa taifa lake na kuunda a well function unit. This coordination ni muhimu sana kwa ujenzi wa taifa lolote.
Hakuna kitu tutachojenga kikawa imara pasipo kujitolea kwetu kwa taifa hili kwa nafasi zetu zote. Hatutaendelea kama hatuna dhamira ya dhati ya kutaka kuendelea kama taifa na ili tuendelea lazima tujenge tabia zinazofaa kwa watu wetu wote. Tabia ambazo zitasababisha taifa hili kuendelea. Tabia zote nzuri kwa kufanya hivyo tutajenga tabia ya nchi yetu na watu wa nje watatutambua kwa tabia zetu. Kwa sasa hakuna consistency katika tabia zetu na tabia ya nchi.
Lazima watu wetu wawe na perseverance na endurance lakini pia lazima wawe na Ideals za aina ya taifa wanalotaka kulijenga. Nature inaunda vitu kutokana na mawazo, vitu vyote tunavyo viona vimetokana na mawazo kila kitu unachokiona kimeundwa na binadamu, hakikuwepo mwanzo kilikuwa hakionekani lakini sasa viko dhahiri machoni kwetu.
Kwahiyo ni lazima tuwe na malengo kama taifa kisha tuyafuate malengo hayo pasipo kukata tamaa kuhakikisha malengo hayo yanatimia. Lakini hili halitowezekana pasipo kuwa na maarifa ya kutosha ya kufikia malengo hayo. Kwahiyo ili tuendelee lazima tu struggle tusilale.
Kuendelea tutaendele tena pengine zaidi ya mataifa mengi lakini inatubidi tuache baadhi ya mambo ambayo ni kikwazo kwetu katika kuendelea na tuwe tayari kutumikia.
Kwasasa tunahitaji a bold leadership ili ku set direction. Tunahitaji matured mind na hii sio lazima awe mzee maturity ya mind inakuja kutokana na kufikiri haiji hivi hivi inakuja kutokana na nidhamu na fikra. Mtu ambaye mwenye uwezo wa kufanya maamuzi yenye mantiki yenye kunufaisha taifa. Mtu asiyeogopa na mwenye uwezo wa kusimamia rational decisions alizofikia after deliberations. A strong man but also wise.