Kwa sifa hizi, kweli tuna waandishi wazuri wa script kwa filamu zetu?

Kwa sifa hizi, kweli tuna waandishi wazuri wa script kwa filamu zetu?

M'bongo

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Posts
265
Reaction score
302
Sinema bora hupimwa kwa vigezo vitano;
mwongozo (script) mzuri, waigizaji wazuri, muongozaji mzuri,
wapigapicha wazuri, na mhariri mzuri. Skripti ndiyo inayoibeba
sinema, na endapo hutakuwa na skripti nzuri iliyotokana na hadithi
nzuri basi ujue kuwa kazi nzima itakosa mwelekeo.

Hadithi ni ramani (kama ilivyo ramani ya nyumba) na script ndiyo
msingi wa nyumba. Kama msingi utakuwa legelege basi sidhani
kama nyumba itasalimika. Ili utambulike kama mwandishi wa script
mwenye taaluma ya uandishi (professional scriptwriter) unapaswa
kuwa na sifa tisa:

-Analytical ability (Uwezo wa kuchambua habari): Lazima uwe na
uwezo wa kugusa mahitaji halisi ya walengwa wako na uwezo wa
kutofautisha mambo muhimu na yasiyo muhimu.

-Interest in diverse topics (Shauku ya kuangazia mada mbalimbali):
Mwongozo mzuri (script) unahitaji utafiti wa kina na makini.

-Organizational skill (Uwezo wa kukusanya taarifa): Uwe na uwezo
wa kuandaa taarifa zenye mantiki kuhusiana na kisa chako.

-Empathy for your audience (Uelewa kwa watazamaji wako):
Lazima uwe uzame ndani ya mitazamo ya watazamaji wako, vitu
wanavyovipenda, mitindo yao, na maslahi yao.

-Writing skill (Ujuzi wa kuandika): Lazima uwe na uwezo wa kuandika
kwa uwazi na kwa ufupi, na lazima uwe na uwezo mzuri katika sarufi.

-Ability to think visually (Uwezo wa kufikiri ): Lazima uwe na uwezo
wa kuwasilisha taarifa yako sambamba mawazo na picha, na si maneno tu.

-Creativity (Ubunifu): Ubunifu katika kufikiri unahitajika kwa ajili ya kuandika
mwongozo (script) wenye mafanikio.

-Presentation and selling skills (Uwezo wa kuwasilisha na kuuza kazi):
Lazima uwe na uwezo wa kuwasilisha mawazo yako kwa ufanisi kwa wateja
wako na uwezo wa kuuza kazi yako.

-Ability to work on a team (Uwezo wa kufanya kazi kitimu): Kiutendaji
utajikuta ukifanya kazi na watu kadhaa wenye kazi tofauti.

SOURCE: Mwanaharakati

 
Nitarudi. Nitarudi pia katika Thread yako iliyopita. Vinginevyo nakubaliana nawe asilimia mia moja. Nitarudi.
 
Nashukuru M'bongo kwa darasa unalotoa hapa. Wenye nia ya kujiifunza watajifunza tu. Tasnia ya filamu hapa Tz inakosa wabunifu, matokeo yake filamu zetu zinakuwa na mtiririko unaofanana sana. Juzi nilikuwa naongea na wasambazaji fulani ambao walikuwa wanalalamika wanashindwa kuuza kwa kuwa filamu zinatoka kwa wakati mmoja na maudhui yanafanana. Watazamaji wakitaka kuzinunua huwa wanawauliza stori iliyomo, wakipewa idea wanachagua filamu moja tu kwa kuwa wanajua zingine zinafanana na waliyoichagua.

Tunahitaji sasa wabunifu muingie katika filamu.

Asante tena kwa thread hii.
 
mkuu umenipa link moja muhimu sana ambayo taarifa zake ndizo ufumbuzi wa tatizo langu. cheki na hapa
 
M'bongo, nadhani hapa umefika. Mimi ni mmoja wa watu wanaopenda sana
kuperuzi mambo yanayohusu tasnia ya filamu. Nitarudi kuchangia ngoja nikajipange vizuri
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Back
Top Bottom