Kwa staili hii tutatoka kweli?

Nitengeneze ya Hoteli au nipotezee tuu

  • Potezea

    Votes: 0 0.0%
  • Tengeneza

    Votes: 4 100.0%
  • Sijui

    Votes: 1 25.0%

  • Total voters
    4
  • Poll closed .

ForeverMore

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2014
Posts
812
Reaction score
1,939

Aisee watanzania sisi tuna matatizo, nadhani ndo maana tuna sua sua kwenye biashara. Baada ya kuangaika sana na mshikaji kutoka US kutafuta gari mitandaoni (shida haswa ni kuwa gari hazina details za kutosha yaani mpaka mpigiane simu sana) nikaamua kutumia elimu yangu kutengeneza website ya kutangaza magari bure. Yaani muuza magari aumizi kichwa, details zote anaweza weka kwa kuweka tick sehemu husika. No hustle.

Tena nikaweka sehemu mbili za ku register yaani kwa muuza gari lake binafsi, na kwa wafanya biashara za kuuza magari (dealers)
Lakini bwana, duu watanzania wavivu, unamweleza mtu anaipenda frsh kabisa ila anataka wewe ndo mpigie picha magari yake na kumwekea mtandaoni. Sasa unajiuliza yaani nikutengeneze website kwa ajili ya wewe kufanya biashara bure kabisa, bado tena nikuweke magari? Really??

Mwingine anakwambia biashara ngumu. haa, yaani haelewi kuwa hiyo ni sababu tosha kutumia hiyo website (www.bongocars.com)

Yaani ni shida. Nikaongeza features kama za kuwasilianza na muuza mgari humo humo kwenye website (messaging) na hata kwa email pia bado ni shida. Picha unaweza weka mpaka ishirini kwa gari moja bado shida.

Alafu nilitaka kuweka sehemu ya kuomba mkopo wa gari, kupata bima ya gari na pia huduma ya kusafiri gari east africa ila kusema kweli nimevunjika moyo.

Kuna maelezo ya kwanini hii website ni nzuri hapa
Bongo Cars - 10 Reasons you should use Bongocars.com

Sasa nataka kutengeneza ya hoteli, guest house, lodge, hostel na hata watu wa tour ili waweze pokea booking na hata malipo online, hii nikutokana na shida ninayoipata (ambayo na nadhani wengi tunapata shida hiyo) ya kusafiri bila kujua utafikia wapi. Hasa pale unapofika usiku.
Ingawa hata ukifika mchana unajikuta umelala sehemu ya bei ya juu au huduma mbaya kwa sababu hujui sehemu nyingine. Ila sina imani na watanzania
Nimejaribu kuandika maelezo yake hapa
Neema kwa wenye Hoteli, Guest house, lodge, hostel, apartments na utalii

kuona kama itapata watu hasa wanojishughulisha na biashara hiyo (nimeweka form ya kujaza) ili nisijitese bure kama ya www.bongocars.com

NB: Naona comments nyingi zina suggest matangazo, naona tufanye hv, ingia kwenye website (www.bongocars.com) utaona icons za kushare, click share kwenye groups za whatsapp, facebook na kadhalika, then nitakuja kuleta mrejesho.
 
Watakuja wauliziaji magar,,ila kwa mtu hapa
 
Yani wabongo bana, hata kucomment tu hapa napo ni shida.....je huko kutuma picha ....
 
Yani wabongo bana, hata kucomment tu hapa napo ni shida.....je huko kutuma picha ....
Yaani, naona sijui kila mmoja anasubiri mpaka wengine waweke magari ndo nayeye aweke. Tunaogopa kuanza... Kwa staili hii hatufiki popote, tutabaki kulalamika tu biashara ngumu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona sioni kitu ndani? Kuna magari used kweli ? Au ya wabongo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe unatakiwa u advertise vizuri na blog iwe simple mtu anayetaka kuuza ajisajiri ila anayenunua awe anaweza kuangalia tu kila kitu baada ya kujirizisha ndo ajisajiri.



Sent using Jamii Forums mobile app
Dah, aisee narudia tena, umesoma thread? Umesoma hizo link nilizoweka? Maana hayo maelezo yote yapo. Na kama ujaona Matangazo kwenye Facebook na Instagram tena yale ya kulipa facebook kabisa sijui umejichimbia wapi
Na hata wewe sasa hivi ukienda www.bongocars.com na hauja jisajiri, kuna kitu usichokiona?
Na pia ku post hauhitaji hata kujisajiri ingawa ukijisajiri unapata features nyingi zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni wazo zuri lakin nazan ukifanya matangazo na kuwaelimisha umuhimu wa kupost kwenye website yako bure wataelewa tu umuhimu wake wa kujitanua kibiashara
 
Ni wazo zuri lakin nazan ukifanya matangazo na kuwaelimisha umuhimu wa kupost kwenye website yako bure wataelewa tu umuhimu wake wa kujitanua kibiashara
Kama matangazo nimefanya haswa, including kuwatembelea kabisa


Unaona matangazo hayo, ndo maana nasema, wanaona, wanaipenda website, tatizo uvivu... Wengi wanashindwa kujiongeza, bado wabataka mteja mpaka akufuate showroom
 
Na pia nimepost sana kwenye magroup ya kuuza magari facebook mpaka nikawa burned na facebook for 4 days nisipost kwenye group lolote. Imagine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi nilitengeneza website kupitia kampuni ya shopify sasa jamaa hawataki malipo ya mwezi kupitia card ya crdb ndo niliyotumia sasa wameifunga website imenikost sana sababu nilishaanza kuipromote na watu kuanza kunielewa sasa kupata card nyingine huku niliko ni mziki card nasubiri miezi mitatu bado haijatengenezwa
 
Hongera
usivunjike moyo
je huo mtandao wako uko na app ya simu?
kama huna naomba uweke
simu ndo kila kitu...na kwa simu ukiwa na app ni easier

usivunjike moyo....hiyo ya hotel ni idea nzuri zaidi..
 
Dah pole sana kaka... Najua how much ina cost, na siyo hela tu, ni muda na malengo uliyokuwa umejiwekea...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera
usivunjike moyo
je huo mtandao wako uko na app ya simu?
kama huna naomba uweke
simu ndo kila kitu...na kwa simu ukiwa na app ni easier

usivunjike moyo....hiyo ya hotel ni idea nzuri zaidi..
Shukran kaka, nilitaka kutengeneza app ya simu pia lakini investment ni kubwa... Na kama nilivyosema imenivunja moyo kuona watu niliyo watengenezea hawaitumii.
Kama wataanza itumia, nitatengeza app ya simu.
Ya hoteli ina cost kubwa pia, kama nitapata atleast watu wahoteli 10 wakaniahidi kuitumia, nitatengeza faster...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…