Kwa Taarifa: Mkinge Mwenza Wako na Rapex

Kwa Taarifa: Mkinge Mwenza Wako na Rapex

Albert Msando

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
1,019
Reaction score
171
Wasalaam,

Sina uhakika kama taarifa hii imewahi kutolewa hapa. Nimewahi kupita ila sijawahi kuishi hapa.

Nchini Afrika ya Kusini kuna Condom ya kike imezinduliwa (muda kidogo umepita)ambayo inasaidia 'wakati wa kubakwa'. Nimesema hivyo kwa sababu aliyegundua anasema inazuia kubakwa lakini hapa kwetu sidhani kama inazuia. Kubaka kwa sheria zetu ni kitendo cha kumuingilia mwanamke bila ridhaa yake na kumuingilia ashakum si matusi ni kuingiza hata 'kichwa'. Hiyo ndiyo sheria.

Condom hiyo inayoitwa Rapex inavaliwa na mwanamke kila atokapo nyumbani na kuelekea maeneo hatarishi. Inachofanya ni mara baada ya mwanaume kuingiza 'anachoingiza' inabana na kumchoma huku ikisbabisha maumivu makali. Ili kuitoa ni lazima aende hospitali kutolewa na condom hiyo inauwezo wa kukusanya DNA ya mbakaji.

Kuna mambo yanayoweza kujitokea au maswali ya kujiuliza;

1. Je kina dada wengine hawatatumia kukomoa?

2. Je mbakaji hatapata hasira na kutenda kosa kubwa zaidi kama mauaji?

3. Condom hiyo inavaliwa kila mara hiyohiyo au inabidi kubadilishwa hata kama mtu hajabakwa?

4. Hapa kwetu itafaa? Lakini mbakaji akishaingiza kisheria si amebaka na aliyebakwa anakuwa ameshabakwa?

Kwa ninavyoona ni vizuri kwa wanaume ukamkinga mwenza wako kwa kumnunulia na kumshauri avae kila mara akienda ofisini kwa bosi wake, akienda kwenye party za wakora, akiwa anakunywa bila kipimo nk. Pia mwanao wa kike inaweza kumsaidia.

Maoni na mawazo tofauti yatasaidia.
 
Jamani wanawake mbona tuna kazi, kisa cha kutembea na jidubwana sekemu za siri? kwa kweli tunapoelekea dunia hii eti hapo unajikinga na binadamu mwenzako. bora lakini, sasa mabikira inakuwaji inapita au ni kwa ajili ya wazoefu tu
 
hapa nchini itatumika kwa kukomoana....

na sijui madhara yake kwa mwanaume yakoje??????????????

duh.?????
 
hapa nchini itatumika kwa kukomoana....

na sijui madhara yake kwa mwanaume yakoje??????????????

duh.?????

Hahahahahaaaa umesikia mumeo anacheat unamvalia tu hiyo ndom, unamkomoaje!sasa badae mtu akiumia ataweza tena kuwa rijali?
 
Hahahahahaaaa umesikia mumeo anacheat unamvalia tu hiyo ndom, unamkomoaje!sasa badae mtu akiumia ataweza tena kuwa rijali?

kwa mke sio sana,but wanawake wa pembeni huwa wana hasira sana
ukiwaaambia basi nataka kutulia na wife,tuachane,wengi wanakuwa washari
ndo yale mambo ya kwenda hata kwamganga,umenipata?????????
 
Hii itakuwa na faida na hasara. Kwa nyumba ndogo itakuwa kukomoana. Ukijidai sasa basi au ukiona invoice zimezidi ukataka kuondoka unakumbana na Rapex at its best. Hospitali lazima utoe maelezo kulikoni ndio utolewe. Ila itakuwa ni hatua nzuri ya maendeleo ingawaje wapo wanaosema uvumbuzi huo unasbabisha mwanamke kujisikia vulnerable muda wote.
 
Back
Top Bottom