Bro usiumize kichwa sana na utopolo utakuwa chizi. Rejea mazungumzo haya baina ya viongozi wa hizi timu mbili.
MAZUNGUMZO 1.
Yanga: Hivi imekuwaje simba anachukua ubingwa mfululizo?
Mshauri: Wachawi tu wale na fitna za nje ya uwanja.
Yanga: Sasa tunafanyaje?
Mshauri: Tuhonge tff, marefa, timu nyingine wawavunje miguu, turoge sanaa, tuwachafulie image yao kimataifa, tuwaharibie dili za wachezaji wanaotaka kuwanunua toka nje, yaani fitna fitna tuu, unasemajejw boss?
Yanga: Safi sana tuanze kazi hii mara moja.
Mshauri: Sawa boss lete mpunga tuingie kazini.
MAZUNGUMZO 2.
Simba: Hivi inakuwa hatufiki fainali mashindano ya kimataifa.
Mshauri: Tujifunze kutoka kwa wengine wamefanikiwa vipi.
Simba: Ok, lete bajeti yako ya kufanya utafiti na uje na majibu yenye mashiko.
Mshauri; Bosi utafiti wangu kwanza inatakiwa kubadili mfumo, Kuwekeza kwa vijana na wazoefu kwa wakati mmoja, kuachana na mtazamo wa kuifunga utopolo tuu, kuachana na mawazo ya kununua gemu, kuelekeza nidhamu kila mtu kwenye nafasi yake na pia kuachana na makocha waujanja ujanja.
Simba: Ok hii ina maana pia tujitathmini sisi wenyewe na sio kujifananisha na timu nyingine za hapa ndani.
Mshauri: Ndio mzee