Kwa Takwimu hizi, CHADEMA bado ni Chama kichanga sana

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Je, wajua kwamba Chadema kwenye kanzi data yao ina wanachama wasiozidi 450,000 nchi nzima.

Hivyo, ukitazama ndani ya miaka 32 ya kufanya siasa nchini CHADEMA inasajili wanachama 14,062 tu kwa mwaka.

Kama utagawanya tena hiyo 14,062 kwa mikoa 26 CHADEMA ina wastani wa wanachama 540 kwa kila mkoa hivyo ukitazama mkoa kama wa Dar es Salaam yenye wakaazi zaidi ya milioni 6, utagundua CHADEMA ina wanachama wachache sana kwa ngazi ya mkona, chini ya asilimia 3

Hapo sijaamua kushuka kwenye ngazi ya wilaya, kata, vitongoji, mitaa na vijiji.

Ni wazi kwaamba CHADEMA bado ni chama kichanga sana licha ya kufanya siasa kwa muda mrefu kidogo lakini ajabu ni kwamba kijitutumua kuonesha ukubwa ambao kimsingi hakina.

Ushauri wangu kwao warudi kwenye drawing board upya kuangalia wanakosea wapi na namna gani wanaweza kurudi tena kwenye kufanya siasa za ushindani.

Na wajue kwamba, kwa makubwa aliyoyafanya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kati ya 2021 - 2024, CCM itashinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu 2025 na hii ni kutokana na matokeo mazuri ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 2024.

USSR
 
..CCM inapokea BILLIONI 3.2 kila mwezi kama ruzuku kutokana na kodi ya Watanzania.
 
Tusikidharau sana hicho chama kwasababu 2020 kilipata kura 1.93m za urais. Ina maana kuna watu ambao sio wanachama wao waliwapigia kura. Mwaka 2010 kupitia Dr Slaa walipata kura 2.2m.. mwaka 2015 siitaji kwasababu ulikuwa uchaguzi wa mwanaCCM dhidi ya mwanaCCM. Tuko kwenye nyakati za uchaguzi hata kura 1 ni muhimu.
 
Jamaa ako USSR akiona hii comment anakuchomoa kwenye group lenu la wasup😀
 
Hapana. Kwenye hizi nyakati za uchaguzi sio poa kudharau mpinzani. Vyama vilivyowahi dharau wapinzani wao hadi nyakati za uchaguzi vilishindwa vibaya. Kwenye uchaguzi lolote hutokea.
 
Hata CHADEMA inapokea ruzuku zinazoishia kutafunwa na Sultani Mbowe.

..ukitaka kujua udogo wa chadema linganisha ruzuku yao na ile wanayopokea ccm.

..kila mwezi ccm wanapokea BILLIONI 3.2 kama ruzuku toka serikalini.
 
Uchanga au Ukomavu wa Chama hautegemei idadi ya wanachama!
Pamoja na kuwa na idadi ndogo ya wanachama bado CHADEMA kinaitesa CCM usiku na mchana.
 
Ndo wafanye siasa zenye ushawishi waingize wabunge wengi bungeni
 
Je wajua kwamba Chadema kwenye kanzi data yao ina wanachama wasiozidi 450,000 nchi nzima.

Hivyo, ukitazama ndani ya miaka 32 ya kufanya siasa nchini CHADEMA inasajili wanachama 14,062 tu kwa mwaka.

Kama utagawanya tena hiyo 14,062 kwa mikoa 26 CHADEMA ina wastani wa wanachama 540 kwa kila mkoa hivyo ukitazama mkoa kama wa Dar es Salaam yenye wakaazi zaidi ya milioni 6, utagundua CHADEMA ina wanachama wachache sana kwa ngazi ya mkona, chini ya asilimia 3

Hapo sijaamua kushuka kwenye ngazi ya wilaya, kata, vitongoji, mitaa na vijiji.

Ni wazi kwaamba CHADEMA bado ni chama kichanga sana licha ya kufanya siasa kwa muda mrefu kidogo lakini ajabu ni kwamba kijitutumua kuonesha ukubwa ambao kimsingi hakina.

Ushauri wangu kwao warudi kwenye drawing board upya kuangalia wanakosea wapi na namna gani wanaweza kurudi tena kwenye kufanya siasa za ushindani.

Na wajue kwamba, kwa makubwa aliyoyafanya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kati ya 2021 - 2024, CCM itashinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu 2025 na hii ni kutokana na matokeo mazuri ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 2024.

USSR
Update hiyo ilikuwa ya mwaka gani? Nauliza hivi Kwa sababu ukienda kwenye websites za baadhi ya wizara utakuta bado information ni ya zamani wakati kumeshafanyika mabadiliko, lakini hayajaingizwa. Mfano, unakuta baadhi ya taarifa zinasomeka ni za mwaka 2020 au kabla wakati leo ni mwaka 2024. Naamini wao wanajua zaidi wako wangapi, kuliko wewe unayesubiri hadi takwimu ziingizwe kwenye mifumo yao ya online. Mfano, wakichelewa ku'update' data zao haina maana au si sawa na kusema hawajapata wanachama wapya. Mfano mzuri ni taarifa za baadhi ya wizara zinazonyesha as if hakuna kilichofanyika, yet katika kila wizara kuna mambo yanafanyika kila siku, kila wiki, kila mawezi na kila mwaka.
 
Tusikidharau sana hicho chama kwasababu 2020 kilipata kura 1.93m za urais. Ina maana kuna watu ambao sio wanachama wao waliwapigia kura. Mwaka 2010 kupitia Dr Slaa walipata kura 2.2m.. mwaka 2015 siitaji kwasababu ulikuwa uchaguzi wa mwanaCCM dhidi ya mwanaCCM. Tuko kwenye nyakati za uchaguzi hata kura 1 ni muhimu.
Hao wamesharudi CCM , walirudi na Lowassa
 
Uchanga au Ukomavu wa Chama hautegemei idadi ya wanachama!
Pamoja na kuwa na idadi ndogo ya wanachama bado CHADEMA kinaitesa CCM usiku na mchana.
Kweli kabisa! Kama Chadema bado ni chama kichanga kisingeweza kudhibitiwa to that extent. Ona tu idadi ya askari walivyojaa Dar es Salaam, na pia mikoani kudhibiti maandamano ya Chadema, halafu mtu aseme hicho ni chama kichanga, kweli? I don't believe it.
 
Je, wajua kwamba Chadema kwenye kanzi data yao ina wanachama wasiozidi 450,000 nchi nzima.

Hivyo, ukitazama ndani ya miaka 32 ya kufanya siasa nchini CHADEMA inasajili wanachama 14,062 tu kwa mwaka.

Kama utagawanya tena hiyo 14,062 kwa mikoa 26 CHADEMA ina wastani wa wanachama 540 kwa kila mkoa hivyo ukitazama mkoa kama wa Dar es Salaam yenye wakaazi zaidi ya milioni 6, utagundua CHADEMA ina wanachama wachache sana kwa ngazi ya mkona, chini ya asilimia 3

Hapo sijaamua kushuka kwenye ngazi ya wilaya, kata, vitongoji, mitaa na vijiji.

Ni wazi kwaamba CHADEMA bado ni chama kichanga sana licha ya kufanya siasa kwa muda mrefu kidogo lakini ajabu ni kwamba kijitutumua kuonesha ukubwa ambao kimsingi hakina.

Ushauri wangu kwao warudi kwenye drawing board upya kuangalia wanakosea wapi na namna gani wanaweza kurudi tena kwenye kufanya siasa za ushindani.

Na wajue kwamba, kwa makubwa aliyoyafanya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kati ya 2021 - 2024, CCM itashinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu 2025 na hii ni kutokana na matokeo mazuri ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 2024.

USSR
Kwa takwimu ni chama onewa sana,kinachowanyima usingizi waonevu
 
Pamoja na uchache wao lakini wanaikosesha usingizi CCM kiasi inatumia jeshi lenye bunduki liwalinde. Idadi ya wanaccm imejaa wanafunzi, wamachinga(hawa mikopo inawalazimisha), wahindi na waarabu tusiowaona kwenye mikutano yao(hawa ni kibiashara na uraia zaidi), walimu na watumishi serikalini(hawa wanalazimishwa) na askari nao pia wanalzimishwa. Wanachama wa upinzani ni wa hiyari ya moyo, hakuna anayelazimisha ili apata mkopo au asamehewe kodi, hata hivyo ni tishio kwa watawala mpaka wanatengeneza mifumo ya wizi wa kura kiasi wafikia kuumbuana wenyewe kwa wenyewe mfano halisi Nape aliyefichua siri mara mbili.
 
Pamoja na Idadi ndogo ya wanachama ila CHADEMA bado mnaiogopa. Mnateka wanachama wake, mnawaua wanachama wake na bado mnawafungulia kesi. Kama kweli CHADEMA ni chama kidogo nadhani Leo tungekuwa na Katiba Mpya au Tume Huru ya uchaguzi. Na Wala hakuna mgombea wa CHADEMA ambaye angeenguliws kwenye uchaguzi.
 
CCM wanaogopa kachama kadogo.Marabook kabisa!
 
Je, wajua kwamba Chadema kwenye kanzi data yao ina wanachama wasiozidi 450,000 nchi nzima.

Hivyo, ukitazama ndani ya miaka 32 ya kufanya siasa nchini CHADEMA inasajili wanachama 14,062 tu kwa mwaka.

Kama utagawanya tena hiyo 14,062 kwa mikoa 26 CHADEMA ina wastani wa wanachama 540 kwa kila mkoa hivyo ukitazama mkoa kama wa Dar es Salaam yenye wakaazi zaidi ya milioni 6, utagundua CHADEMA ina wanachama wachache sana kwa ngazi ya mkona, chini ya asilimia 3

Hapo sijaamua kushuka kwenye ngazi ya wilaya, kata, vitongoji, mitaa na vijiji.

Ni wazi kwaamba CHADEMA bado ni chama kichanga sana licha ya kufanya siasa kwa muda mrefu kidogo lakini ajabu ni kwamba kijitutumua kuonesha ukubwa ambao kimsingi hakina.

Ushauri wangu kwao warudi kwenye drawing board upya kuangalia wanakosea wapi na namna gani wanaweza kurudi tena kwenye kufanya siasa za ushindani.

Na wajue kwamba, kwa makubwa aliyoyafanya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kati ya 2021 - 2024, CCM itashinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu 2025 na hii ni kutokana na matokeo mazuri ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 2024.

USSR
Wewe lazima utakuwa mtu jangili wa kisiasa kama unafurahia vitendo vya hovyo vya CCM katika nchi hii.
 
Nadhani Kuna wanachama, wafuasi na mashabiki! Ukijua hili utagundua Kuna watu wanakisapoti sio Kwa sababu ni wanachama Ila ni wafuasi au mashabiki! Asante
 
Back
Top Bottom