Kwa tulio ‘ Masikini ‘ ni kweli haya yanatuhusu au wanatusingizia tu?

Kwa tulio ‘ Masikini ‘ ni kweli haya yanatuhusu au wanatusingizia tu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
1. Viatu huisha upande mmoja

2. Lazima awe shabiki wa _*YANGA*_

3. Hunywea maji kwenye jagi hata kama kuna glass au kikombe

4. Kupenda kuvaa suruali zenye rangi ya kung'aa.

5. Kufungua soda kwa meno

6. Kuvaa socks hadi magotini hata kama hayupo mazoezini

7. Anapenda sana kuangalia movie zilizotafsiriwa

8. Kufuta jasho kwa vidole

9. Kupiga miayo hadi machozi yanamtoka.

10. Kuingilia ugomvi hata wa watoto wadogo

11. Kumchukia kila mwanamke anayemiliki gari

12.Kumiliki smartphone iliyopasuka kioo.

13.Akitengewa chakula lazima amalizie kunywa mpaka na mchuzi kwenye kibakuli.

14.Kila mwanamke anayemchangamkia kwake anajua ashapata zari la kupendwa.

15.Wanapenda sana kutafuna vitumbua asubuhi asubuhi bila chai.

16.Akiingia kuoga bafuni, anahakikisha anasugua mpaka ndala akiamini usafi huficha umasikini.

17.Akipanda dala dala lazima ashike nauli mkononi ili isije kudondoka.

18.Wanapendaga sana kukaa siti za dirishani kwenye safari yoyote.

19.Ukiangalia mashati yake mengi utakuta kola za mashati zimeanza kuchanika.

20. Akiingia tu JamiiForums huwa anaichukia sana na mno tena pasipo sababu yoyote ile ID ya GENTAMYCINE.
 
Hilo namba 9 la kupiga miayo na machozi kutoka linaweza kumtokea yeyote yule.

Sababu ni kuwa, wakati wa kupiga miayo kuna misuli katika uso hukakamaa ambapo husababisha tezi maalumu zinazozalisha machozi kupata mbinyo kidogo ndipo 'tuchozi tudogo' hutolewa.
 
No. 20 ndio umeandika pumba OG kuliko pumba 1-19
 
No. 20 ndio umeandika pumba OG kuliko pumba 1-19

Hili Jibu lako tu hapa limenithibitishia kuwa Wewe si tu Masikini wa Kipato bali hata Umasikini wa Akili unao na ' Umekutukuka ' kabisa.
 
Hahahaaa ila watu mnajua kumuotea mtu! Hizo sio sifa za maskini ila ni sifa zetu watanzania
 
Ile id nyingine si wamekuunga nayo? Nashauri fungua nyingine.

Ila bro kujifanya una akili nyingi jambo dogo tu la kuficha id zako limekushinda?
 
Back
Top Bottom