Kwa ufaulu huu wa Hisabati wa 19.54% tutarajie wachumi kuwa janga la taifa

Kwa ufaulu huu wa Hisabati wa 19.54% tutarajie wachumi kuwa janga la taifa

Mbogi

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2021
Posts
803
Reaction score
997
Somo hili limekuwa na matokeo mabaya si kwa shule za sekondari tu bali pia hata shule za msingi, kwa miaka zaidi ya sita iliyopita wameendelea kutuaminisha kuwa ufaulu umeongezeka kila mwaka,yawezekana lakini kwa asilimia hizo ni hatari.

Jambo la kusikitisha Sana hakuna jitihada za maksudi zinazotekelezwa na serikali katika kuondokana na tatizo hili.

Serikali iwaajili walimu wa sekondari wa somo hilo ambao kwa miaka mitano hawakuajiliwa ili wakaongeze nguvu na kuziba pengo la walimu wengi waliostaafu. Kwa sasa mwalimu mmoja anaweza kuwa anafundisha kitato cha 1 hadi cha nne mikondo a hadi c.

Na walimu wa shule za msingi waliopo kwa sasa waongezwe maarifa na mbinu nzuri zaidi za ufundishaji wa somo hili kupitia kozi fupifupi kwa awamu. Lakini pia huko nako walimu waajiliwe.

Majengo mengi yaliyojengwa yaendane na utoshelevu wa walimu hasa wa hisabati.
 
Hesabu ni janga la kitaifa jitihada kwa serikali inaitajika sana
 
Somo hili limekuwa na matokeo mabaya si kwa shule za sekondari tu bali pia hata shule za msingi, kwa miaka zaidi ya sita iliyopita wameendelea kutuaminisha kuwa ufaulu umeongezeka kila mwaka,yawezekana lakini kwa asilimia hizo ni hatari.
Tuanze na wewe,ukipata ngapi kwanza
 
Taifa ambalo halitakuwa na engineers, scientist na technologists.....baadala yake litakuwa jalala la bidhaa kutoka kila pembe ya dunia na watalaam kutoka India, China na ughaibuni kwingine...
 
Mtoto anakula sembe, soseji, eggchop sijui, ufresh twist nk utegemee awe na akili ya kushika kitu kichwani lishe duni inaathiri ubongo lazima uone hesabu ngumu

Wazazi wafundishwe kuwapa watoto chakula bora huo ukisasa wanaodhani ndiyo ujanja unawaathiri watoto, wawape mboga za majani kwa wingi, matunda, karanga na wenzake kina korosho na vyakula vingine hivi vya asili na kuwapa muda wa kucheza siyo muda wote ni homework vitawasaidia watoto
 
That is 80.46% Failure
Yaani ni hatari Sana kwa sababu, ukifuatilia kwa undani zaidi katika hizo 19.54% utaona kuwa zaidi ya 15% walipata daraja D ambalo nalo si zuri.

Kwa maana nyingine ni kuwa hadi sasa kutoka miaka sita iliyopita ambapo wanafunzi wamekuwa wakipata ufaulu wa pungufu ya 19% tunao upungufu mkubwa sana wa walimu wa somo hilo ama walio vyuoni au mitaani.

Hata hivyo wasiwasi unakuwa mkubwa zaidi katika kuwaamini watendaji na wataalam wetu katika kutoa miongozo ya kitaalam kama vile kupanga, kuratibu na kujenga uchumi, wahandisi wa majengo nk, na ndiyo sasa tunagundua kuwa huenda Ndiyo sababu inayochangia kwa sasa uteuzi wa wataalam ktk sekta inayohusisha hisabati kurudia rudia sura zilezile za zamani na hata wanaostahili kustaafu.
 
Mtoto anakula sembe, soseji, eggchop sijui, ufresh twist nk utegemee awe na akili ya kushika kitu kichwani lishe duni inaathiri ubongo lazima uone hesabu ngumu

Wazazi wafundishwe kuwapa watoto chakula bora huo ukisasa wanaodhani ndiyo ujanja unawaathiri watoto, wawape mboga za majani kwa wingi, matunda, karanga na wenzake kina korosho na vyakula vingine hivi vya asili na kuwapa muda wa kucheza siyo muda wote ni homework vitawasaidia watoto
Hawa wanaokula soseji, eggchop, twist, ni watoto wa kipato cha juu ambao ni wachache na pengine huenda ndio wengi ktka hiyo 19.54%.

Asilimia nyingi za Wananchi ni wa kipato cha chini ambao mwanafunzi hupata mlo mmoja.

Katika suala lishe mashuleni serikali inao wajibu mkubwa wa kuweka utaratibu mzuri wa kuiwezesha shule kupata mlokamili wa mchana kwa kuongeza fedha kidogo za ruzuku na kuweka utaratibu mzuri wa ushirikishwaji na usimamizi kutoka kwa jamii husika. Mkoa wa Kilimanjaro unaweza kutoa mwanga wa ufanisi wa hili.
 
Back
Top Bottom