kwa ujenzi wa maghorofa haya tutegemee maafa mengi

incharge

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2011
Posts
5,017
Reaction score
8,442
nimebahatika kumiliki kiwanja kwenye potential area hapa dar-es-salaam , ukweli ni kwamba serikali lazima ichukue hatua madhubuti sana ili kuzuia maafa mengine yasitokee, wafanyabiashara wengi niliofanya nao mazungumzo kuhusu joint venture wote walisisitiza kwamba engineer ni wa kwake na hataki nilete engineer wangu hata kuhakiki mradi, ukifikiria mara mbili kama muelewa ni wazi kwamba kuna kitu kinachakachuliwa kwenye ubora wa mradi,
kikubwa zaidi nina jirani yangu ameingia ubia na mfanyabiashara mmoja kwenye ujenzi wa ghorofa, lakini kutokana na maelezo ya mtaalamu wake wa ujenzi kwamba vifaa vinavyotumika kama matofali hayana ubora , na kwamba hela inaongea.....
jamani tutateketea kwa mtindo huu, mamlaka husika zianze kufuatilia ubora wa majengo haswa maeneo ya obay, upanga, na kariakoo ambapo kuna utitiri wa maghorofa kuhakiki ubora.​
 
Tatizo nchi yetu ina kitu wanaita Ad-hoc planning. na hii ni sehemu ya utamaduni wetu. ukiuliza kabla ya maafa utasikia serikali inajiaanda kuandaa mchakato ambao ulikuwepo wa kuanza kusimamia na ifikapo mwezi wa 12 mwakani, tutakuwa tayari tumesha blah blah blah.. na baada ya janga kutokea utasikia serikali imeunda tume itakayokuwa huru yenye watu wenye sifa na uadilifu mkubwa kwaajili ya kuchunguza kilichotumika kuchunguza na kusimamia uchunguzi blah blah blah..
baaada ya miezi mingi kupita hakuna majibu ya tume.
:A S confused::A S confused::A S confused:
 
Mkuu, ni kweli kabisa. Ile ripoti ya kamati ya Lowassa nadhani haikufantiwa kazi ndio maana haya yanajirudia.
 
yaani ukipita kariakoo ndiyo aibu kuna maghorofa mengine hata kupita chini yake mtu unaogopa yapo so weak na hamna mtu anaeuliza ila ikitokea tatizo ndiyo kila mtu anamtupia mpira mwenzake mchechu siyo wa kuongea anachokiongea leo amejishushia sana heshima kwa jambo lililotokea, nimeona kariakoo kuna nyumba ina ghorofa 12 na haina lift hii ni sawa kweli kitaalam?
 

kwa kariakoo, Jengo lililojengwa kwa ubora ni soko la kariakoo tu, zingine ni kama vibanda vya kufugia kuku. Tetemeko hata la 3.5 likitokea pale yatatokea maafa na hasara ya kutisha.
 
mamlaka husika
wanapaswa kua makini na sio kutoa vibali
kwa kila mkandarasi khaaa!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…