Kwa Undani kuhusu nguvu za kiume.

Joined
Aug 11, 2017
Posts
61
Reaction score
78
Tatizo la nguvu za kiume.

Upungufu wa nguvu za kiume ni
ugonjwa ambao mwanaume
hushindwa kusimamisha uume na pia kushindwa kuendelea kubaki imara wakati wa tendo la ndoa.

Uume kusimama hutokea pale damu inapoingia katika tishu zilizo kama sponji na kuendelea kubaki ndani yake wakati wa tendo la ndoa.

Hii hutokea kama matokeo ya mhemko kabla ya tendo la ndoa, ambapo taarifa hupelekwa kwenye ubongo na hatimaye taarifa hutumwa katika mishipa ya fahamu iliyo katika uume.

Sababu zinazosabisha tatizo hili
zaweza kugawanywa kama
ifuatavyo:

a.)Hitilafu katika ogani za
mwili(Organic causes ).

Hitilafu hizi ambazo zinatambulika
zaidi ni kama magonjwa ya moyo na
kisukari,upungufu wa homoni mwilini(kitaalam kama
hypogonadism ),maudhi yasiyotakiwa ya dawa mbalimbali
( side effects ),pia magonjwa ya mishipa ya fahamu yanayoweza kusababishwa na kuumia au kufanyiwa operesheni ya tezi dume.

Pia zifuatazo ni sababu nyingine
katika kundi hili.

[emoji117]Kuziba kwa mishipa ya damu.

[emoji117]Kiwango kikubwa cha lehemu katika damu.

[emoji117]Unene (Obesity).

[emoji117]Kukosa usingizi.

[emoji117]Unywaji pombe.


[emoji117]madawa ya kulevya.

[emoji117]Utumiaji wa tumbaku.

[emoji117]Kuumia kwa uti wa mgongo.

[emoji117]Magonjwa ya mmeng’enyo.


b)Matatizo ya kisailolojia.

Ubongo huwa na kazi maalum ya
kuongoza jinsi viungo vya mwili
vinavyofanya kazi, hii ni pamoja na
kusimama kwa uume baada ya
mhemko kabla ya tendo la ndoa.

Kuna baadhi ya mambo yaweza
kusababisha mwanaume asihemke na kuendelea kusababisha tatizo kuwa kubwa zaidi.

Sababu hizo ni kama ifuatavyo:

[emoji117]wasiwasi na hata magonjwa mengine yanayoathiri afya ya akili.

[emoji117]Msongo wa mawazo.

[emoji117]Matatizo ya uhusiano ambayo
hupelekea msongo wa mawazo,
hata mawasiliano yaliyo duni.


c)Mchanganyiko wa hitilafu katika Ogani na Saikolojia kwa pamoja.

Tunavyoozeeka tatizo hili laweza
kuongezeka, ingawa siyo hali ya
kawaida mtu anapozeeka. Wazee ni
kundi ambalo hutumia dawa za
matatizo mbalimbali kwa wingi.

Kwa hiyo tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume linapotokea mara nyingi huashiria hali ya kiafya isiyo ya kawaida au kusababishwa na aina fulani za dawa atumiazo mgonjwa. Mara nyingi hutokea kwa wale walio na miaka 60 na
kuendelea.

Hata hivyo vijana huweza pia kupata tatizo hili.

Pia wanaoweza kupata tatizo hili ni
kama:

Wenye matatizo ya kiafya,
kama ugonjwa wa kisukari na ugonjwa wa moyo.

Wenye kuendesha baiskeli kwa muda mrefu,uendeshaji wa baiskeli
bila kutumia vifaa maalum waweza
kusababisha kukandamizwa kwa
mishipa ya fahamu na kuathiri
mzunguko wa damu katika uume.

Watumiaji wa dawa za kulevya
pamoja na pombe.

Wenye msongo wa mawazo,na wasiwasi.

Wenye kutumia aina mbalimbali za dawa.

Waliojeruhiwa,hususan mishipa ya
fahamu husika.

Wenye uzito mkubwa,hasa walio
wanene.

Wenye kutumia tumbaku,ambayo huathiri mtiririko wa damu katika mishipa ya uume ya ateri na
veini.

Kutoridhika katika uhusiano.

Msongo wa mawazo na wasiwasi.

Kujisikia vibaya mbele ya jamii na kutokujiamini.

Matatizo ya uhusiano au kuvunjika kwa uhusiano.

Kutokuwa na uwezo wa kumpa ujauzito mwanamke.

Endapo tatizo hili litajitokeza,
usikimbilie kuanza kutumia dawa, au kununua dawa katika famasi bila
ushauri wa daktari.

Dawa hazitakuwa na msaada endapo chanzo cha tatizo
hakijagundulika.

Pia matumizi ya dawa yanaweza kukuletea athari nyingine kiafya, kama uchunguzi haukufanyika kwanza.

Jiandae kumwona daktari wako, kwa kukusanya taarifa mbalimbali kama dalili za ugonjwa ulizo nazo, listi ya dawa unazotumia, uwe na taarifa muhimu za kukuhu tatizo lako,na andaa maswali utakayomuuliza daktari wako.

Kwa tiba na ushauri piga simu. 0620144253.

Jiunge sasa na Chuo chetu kwa njia ya Whatsapp,Kwa Ada ya 2000/Kwa mwezi Upate Elimu ya Tiba Asili.

Wasiliana na Dr.Seifu.dodoma.
0620144253./0769116206.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Punyeto mbona haipo hapo? Au ni uzushi wa watu kuichafua Chaputa
 
Kazi kwenu wale wa Daslam......[emoji12] [emoji12]
 
Katika waliowai kuelezea hii kitu wew umejitahid sana,uki right,weng wanakuaga na stor za mitaani,pia huishambulia chaputa wakat chaputa haina uhusiano wowote na hzo nguv.big up sana..chaputa hupunguza nyege tuu vilevile kama unapofanya tendo,so sio sababu.nashukuru kwa ku i save chaputa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…