KWA UOZO ULIOPO NECTA; Ponda aliona mbali kuanzisha movement ya kumn'goa Ndalichako


Mkuu, nakubaliana nawe. Tatizo letu Watanzania tumezoea kudanganywa. Kwahiyo, jamaa anataka Ndalichako na timu yake wangewafaulisha wanafunzi wote hata kama wamefeli ndipo ingekuwa sawa kwa Watanzania tulio wengi. Nashukuru NECTA wamesema ukweli unao uma muda mfupi na ambao utatufanya tufanye mabadiliko kuliko wangesema uongo baadae tuje kuumia muda mrefu!
 
[ hebu soma hii toka Tanzania Daima ndo utaja Necta hawapo makini na kuna uozo na PONDA yupo sahihi

WAKATI mjadala wa matokeo mabaya ya kidato cha nne ukiendelea kulitikisa taifa, kashfa mpya ya matokeo hayo imeibuliwa.
Kashfa hiyo mpya imeibuliwa na Mkurugenzi wa Shule ya Green Acres, Julian Bujugo, kwamba matokeo ya baadhi ya shule nchini ikiwamo yake yamechakachuliwa.
Akizungumza na gazeti hili jana, Bujugoalisema kuwa baadhi ya wanafunzi kwenye shule yake hawakufanya mitihani ya kidato cha nne, lakini matokeo yanaonesha wamefaulu kwa kupata alama za juu.
Alitaja mfano wa mwanafunzi, Humphrey Sanga, mwenye namba 01197/148, ambaye hakufanya mitihani hiyo lakini matokeo yanaonesha amefaulu kwa kupata alama nzuri.
“Huyu mwanafunzi tulimsimamisha na hakufanya mitihani, lakini matokeo yake yanaonekana amepata hivi; Civics D, Historia D, Jiografia C, Kiswahili D, English C, Physics D, Chemistry C, BiologyC, Basic Mathematics D, ambapo amepata daraja la tatu pointi 24,” alisema Bujugo.
Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya ‘Arts’.
Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alamaza masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa.
Alimtaja mwanafunzi mwingine aliyefanya mtihani huo lakini matokeo yake yanaonesha amewekewa ‘absent’ na mwanafunzi mwingine, Mbazi Volta, hakufanya mitihani lakini amepewa alama za ufaulu.
“Matokeo hayo yananipa wasiwasi kwamba yanaweza kuwa yamechakachuliwa,” alisema Bujugo.
Mkurugenzi huyo anaiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kurudia kusahihisha mitihani hiyo ili kuondoa ukungu ulioligubika taifa kwa sasa kuhusu matokeo ya kidato cha nne.
“Naomba usahihishaji urudiwe, maana huu ni ubabaishaji mkubwa…matokeo hayo yamewaathiri watoto kisaikolojia na sijui watakwenda wapi?,” alihoji.
Alisisitiza kuwa usahihishaji urudiwe kwani katika shule hiyo wanafunzi wenye uwezo mkubwa tangu walipoanza kidato cha kwanza ndio waliofanya vibaya wakati waliokuwa wakifanya vibaya, wameibuka na alamaza juu.
Mkurugenzi huyo alisema wazazi wa watoto hao wanatarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki hii kujadiliana kuhusu matokeo hayo na hatua za kuchukua.
Akitolea ufafanuzi suala hilo, Msemaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), John Nchimbi, alisema si kweli kuwa matokeo hayo yamechakachuliwa bali ni matokeo halisi ya shule hiyo.
Alisema iwapo mkurugenzi wa shule hiyo ana shaka na matokeo hayo, alitakiwa kufika katika ofisi za baraza hilo ili apatiwe taarifa sahihi kabla ya kutoa taarifa katika vyombo vya habari.
“Mi nimeangalia hayo majina, naona yapo sawa na hata huyo mwanafunzi ambaye anasemekana hakufanya mitihani na akapewa alama…napenda kusema kuwa alama alizopewa si zake na hata katika orodha yetu anaonekana kuwa hakufanya mitihani,” alisema.
Katika hatua nyingine, Waziri wa wizarahiyo, Dk. Shukuru Kawambwa na wenzake, wamekuwa bubu kueleza endapo wako tayari kujiuzulu au la.
Tanzania Daima ilifika wizarani hapo jana kutaka kuonana na Waziri Kawambwa ili atoe msimamo wake, mwandishi alijibiwa kuwa waziri huyo alikuwa kikaoni na asingeweza kutoka.
Hata waziri alipopigiwa simu pamoja nakutumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakupokea wala kujibu ujumbe huo.
Kwa upande wake, katibu mkuu wa wizara hiyo naye hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa alikuwa kikaoni.
Naye Naibu Waziri, Philipo Mulugo, alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi kueleza msimamo wake, simu yake iliita bila kupokewa na hata hakuwa tayari kujibu meseji ya ujumbe mfupi.
UOTE][/QUOTE]
 
Ponda ni nani?Kama nani kuona uozo?Uozo wa elimu kwenye wizara badala ya kuanzia kwanza kwake mwenyewe na kwa waamini wenzake?

Elimu imefanywa kuwa janga kama majanga mengine.Huu ni mwanzo wa mabaya makubwa yafuatayo punde na baadaye.

Muda wa kubwabwaja umeisha,tutende ili kuibadili Tanzania yetu na wazao wa baadae...!
 
Ponda na mambo ya elimu dunia wapi na wapi? Kwanza anaelewa hata NECTA ni dude gani?!
 
Mpaka pale walimu watakapo thaminiwa na kupewa haki zao za msingi kama teaching allowance, nyumba, mshahara toshelevu nk ndio hii hali itapungua kama si kuondoka kabisa. Otherwise tutaendelea na ma zero kila mwaka.

Huu ndio ukweli ambao viongozi wa serikali na wananchi walio wengi hawataki kuusikia. Wengi utawasikia wakidai kuwa nchi haina mtaala, as if mitihani sijui inatungwa kutoka wapi? wengine wanajidanya kwenye COMPETENCE BASED curriculum, as if waalimu wa shule kama St. Francis wao walisoma vyuo vya nje! Kazi kweli, wananchi waamke, wabaini kuwa watoto wao ndio wanao umia na kufeli huku na wasitegemee mwalimu kujitolea kufanya kazi kama zamani walipoaminishwa kuwa ualimu ni wito kitu ambacho sasa kimetoweka kabisa kwenye akili za waalimu. Waalimu wapo busy kutafuta maisha OUT OF THEIR PROFESSIONAL, so wanafunzi wanajikatia notes darasani. Ngoja tusubiri next year!!!
 
Ndalichako hana makosa kabisa hapa!! Angechelewesha kutoa matokeo hapo angekua na makosa!!
 
Mbona kuhusu haya ya Bujugo jibu lilishatolewa? Mambo mengine tunapenda kulaumu bila kufikirisha vichwa. Hivi Ndalichako ndo mfumo wa elimu nchi hii. Ndo anaajiri walimu, ndo anayetakiwa kujenga maabara na kuleta vifaa vya mabaabara, ndo anayepeleka vitabu vya kiada na ziada, ndo anawasimamia walimu wafundishe, ndiye anawahimiza wazazi wawajibikie elimu ya watoto wao, ndiye anawajibu wa kuwaambia wanafunzi watie bidii katika masomo yao, ndo anatakiwa awajazie wanafunzi majibu ya mitihani ya sayansi ambayo hawakuwahi kuwa na walimu tangu walipoanza kidato cha kwanza, ndo anayetakiwa kufanya ukaguzi wa shule kuangalia ubora wa elimu? au kazi ya NECTA ni ipi? Tujibu maswali hayo kisha tutoe hukumu kwa NECTA. Si mlionyeshwa vijana wanaandika mashairi ya bongo fleva badala ya kujibu maswali waliyoulizwa?Au hamkusikia vile vile kuwa booklet za majibu zilikuwa zinaandikwa namba tu za mtahiniwa bila kujibiwa kitu chochote.Tusichanganye dini, ushabiki, siasa na elimu.
 
Sheikh Ponda kwisha habari yake, yeye makazi yake ya kudumu sasa hivi ni jela , kwahiyo kwa Lugha fupi ni kwamba ameng'olewa yeye.
 
Kiona mbali chako Ponda aenziwe kwa kupewa Ukatibu mtendaji wa Baraza la Mitihani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…