Kwa upepo wa kisiasa ulivyo nchini ni kwanini tusikubali kuwa tuna chama kimoja tu ili mabeberu waingilie kati!?

Kwa upepo wa kisiasa ulivyo nchini ni kwanini tusikubali kuwa tuna chama kimoja tu ili mabeberu waingilie kati!?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Hii hali ya kujidanganya kwamba Tanzania tuna mfumo wa vyama vingi kunatupotezea muda wa kupata demokrasia halisi ya vyama vingi, mimi nishauri hivi vyama vilivyopo vingekubaliana kuweka mpira kwapani ili dunia nzima ijue kuwa serikali ya Tanzania haina nia ya kuruhusu upinzani.

Kuna namna nyingi ambayo serikali yetu inatamani kuidanganya dunia kuwa nchini kwetu kuna demokrasia ya vyama vingi wakati sio kweli hata kidogo.

Yaani kwa mwenye akili yeyote anajua kuwa chama tawala kinahodhi kila kitu, yaani kama ni nyama basi ccm wanafaidi minofu yote kisha wapinzani wanaachiwa vimchuzi na mifupa ili kuidanganya dunia kuwa eti kuna usawa mbele ya bakuli la supu.
 
Mbowe na wenzake ndio wanashindwa kufanya hivyo.
Mimi niliona vivyo hivyo, CDM ivishawishi vyama vingine kisha waombe hati ya kufutwa vyama vyao na msajili. Kwakuwa msajili na CCM ni vilaza watafuta kwa haraka watakapokuja kushtuka washachelewa
Hapo ndipo mwanzo wa siasa mpya Tanzania
 
Usimwamini binadam ambaye anamiliki resources.......
 
Mbowe na wenzake ndio wanashindwa kufanya hivyo.
Mimi niliona vivyo hivyo, CDM ivishawishi vyama vingine kisha waombe hati ya kufutwa vyama vyao na msajili. Kwakuwa msajili na CCM ni vilaza watafuta kwa haraka watakapokuja kushtuka washachelewa
Hapo ndipo mwanzo wa siasa mpya Tanzania
Ni kwa nini shutuma nyingi unazuekekeza kwa Mbowe!?
 
Kwani hivi vyama pinzani alivianzisha nani ? Na kwa lengo gani ?,Walio vianzisha walitokea wapi ?,
 
ni wazo zuli sana nahisi ingekuwa njia sahihi sana mana kwakweli wapinzan wamemezwa,, ila kwa hivi vyama vya upinzani haitawezekana mana wao kwao ni kama mladi wa kuingizia kipato! mana sidhani kama wapo tayali kuyakosa mafweza ya ludhuku!!
 
CCM ina mbinu 9999 za kushinda uchaguzi. Hata huo utitiri wa vyama vya upinzani ni mbinu namba 177 ya CCM.
 
Sasa si wataunda chama cha upinzani cha mchongo tu. Au watawapa wapinzani uchwara chochote kitu mambo yataenda.
 
Sasa si wataunda chama cha upinzani cha mchongo tu. Au watawapa wapinzani uchwara chochote kitu mambo yataenda.
Nadhani hivi nduvyo ilivyo sasa kwa hiyo ili kudai mwelekeo mpya wa siasa za Tanzania yaani lazima turudi kudai demokrasia ya vyama vingi kama ilivyokua miaka ya 1980-90
 
Back
Top Bottom