Kwa ushirikina huu wa Kufuru uliofanyika uwanja wa Karume mkoani Mara tunaelekea kubaya

Kwa ushirikina huu wa Kufuru uliofanyika uwanja wa Karume mkoani Mara tunaelekea kubaya

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Leo huko Mkoani Mara katika Mji wa Musoma ndani ya Uwanja wa Karume kunaenda kufanyika mchezo wa kukata na shoka kabisa wa Ligi daraja la Kwanza baina ya Timu ya Biashara United ya Mkoani Mara na Alliance FC ya Mkoani Mwanza ambapo mshindi wa hiyo mechi ndiyo atakuwa na nafasi kubwa ya Kupanda Ligi Kuu ya Tanzania bara ya Vodacom.

Katika kuelekea ' mtanange ' huu siku ya jana huko Mkoani Mara pale pale mjini Musoma kulifanyika ' vituko ' ambavyo sidhani kama vinastahili kufanyika hasa tunapojitahidi kuliinua soka letu na kukimbizana na Wenzetu waliotuacha kama siyo kututangulia.

Kituko cha Kwanza

Katika maajabu ya mwaka siku zote Timu mgeni hurusiwa kutumia uwanja siku moja kabla ya mechi ili kuuzoea na mara nyingi hutakiwa kuutumia katika session ya asubuhi na ya jioni lakini kwa jana Timu ya Alliance ya Mkoni Mwanza iliruhusiwa kufanya mazoezi yake mara moja tu tena Saa 5 asubuhi na walipewa muda mchache sana na jioni inasemekana hawakufanya mazoezi.

Kituko cha Pili

Jioni mida ya Saa 11 kuelekea Saa 12 kuliingia Kundi kubwa la Watu hapo ambapo lilienda moja kwa moja katikati ya Uwanja huo wa Karume na kufanya ' Ushirikina ' ambao kusema ukweli ni wa ' Kufuru ' kabisa ambako inasemekana walifukia ' Kiungo ' cha wale wanaotetewa kila siku na Shirika la ' Under the Same Sun ' na wakaondoka zao.

Kituko cha Tatu

Usiku muda wa Saa 1 na nusu kuelekea Saa 2 hapo tena kuna Kundi la Watu liliingia na Safari hii liliruka ukuta unaopakana na lile Geti la Kaskazini mwa Uwanja wa Karume likiwa na Mbuzi Mweusi ambaye inasemekena walimchinja mule mule ndani na kwenda nae katika kila Goli la Uwanja ule na kumwaga damu yake na kufukia haraka haraka ili ishara za damu zisibaki na wakaondoka zao.

Kituko cha Nne

Usiku mida ya Saa 3 hapo kuelekea Saa 4 kama kawaida Kundi jingine Kubwa la Watu liliingia tena kupitia Geti kubwa kabisa na kwenda katikati ya Uwanja na bila haya, uwoga wala aibu likachoma moto Kanzu ya rangi Nyekundu na kuondoka zao haraka.

Kituko cha Tano

Na hiki Kituko ndicho kimenifanya GENTAMYCINE nishikwe na hasira kwani si Kitendo cha Kiungwana hata kidogo na kimeniumiza na kunisikitisha mno. Alfajiri hii hii mida ya Saa 11 kuna Kundi la Watu limeenda katika Hospitali moja hapo mjini Musoma na kuchukua Maiti inayosemekana ni ya Mtoto mchanga kabisa na kuifanyia ' ndumba / shirki ' kisha kuondoka nayo na kuirudisha Mortuary ilipokuwa.

CHA KUSHANGAZA

Pamoja na kwamba Vituko vyote hivi vinafanyika ila hadi hivi sasa haijajulikana kwamba walioanya hivyo ni nani kati ya hizi Timu mbili ' hasimu ' kabisa za Biashara United ya Mkoani Mara au Alliance FC ya Mkoani Mwanza ila katika mchezo huo ambao unapigwa leo ndani ya Uwanja wa Karume kuna uwezekano Watazamaji wakawa wanadhani wanaowaangalia ni Wachezaji Binadamu kumbe ' Kiuhalisia ' wanaowatizama na wanaocheza ni Wachezaji Majini tupu.

OMBI

Naiomba Serikali kupitia Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dkt. Mwakyembe na Jeshi la Police la Mkoa wa Mara pamoja na Shirikisho la Soka nchini TFF limkamate upesi sana Meneja wa Uwanja huo wa Karume pamoja, Viongozi wa hizo Timu mbili na hasa Manahodha wake ili wawape ushirikiano kwani inasemekana kuna ' Kiungo ' cha Binadamu kimefukiwa katika Goli moja wapo kisha wafanye Upelelezi wao katika Hospitali ya Mkoa wa Mara juu ya kutolewa kwa Maiti ya Mtoto mchanga na kwenda kufanyiwa ushirikina hapo Uwanjani Karume.

Kwa ' Upuuzi ' huu Tanzania tuna safari ndefu sana ya kupata maendeleo ya Soka.

Nawasilisha.
 
Mh..., inamaana bado "bino" wanauawa/ wanakatwa viungo?
 
Hakuna chochote, hiyo ni kuwaaribu tu kisaikolojia wapinzani wako, yanafanywa sana hayo nchi za kasakazini na magharibi mwa afrika.
 
Una akili ndogo hakuna ushirikina ktk mpira ingekuwa hivyo taifa stars tungechukua kombe la dunia

Sasa Mimi kuwa na akili ndogo na hiki nilichokiripoti hapa Kwenu vina uhusiano gani? Kama nilivyosema kwamba mwaka huu wa 2018 sihitaji Kumtukana Mtu na nataka niwe GENTAMYCINE mpya Kimaadili hivyo kwa ' tusi ' lako hilo Kwangu niseme tu asante sana na kama bado una hamu au unajisikia kuendelea Kunitukana kuwa huru tu Mkuu. Mungu akusamehe na akupe rehema ya Hekima na Busara.
 
Ndo africa yetu bna
Wanaamini sana katika uchawi ndo maana hawaendelei
 
Una uthibitisho wowote usio na shaka juu ya vituko tajwa? KV.picha, video n.k?
 
Mida yote umekua shuhuda wa matukio hayo machafu
Hongera sana unafaa saana

Waafrica. Ndivyo tulivyo
 
Haya mambo ya mpira haya yanaumizaga sana ukiyafuatilia lakini ni kweli haya mambo yapo,Hizi mechi za mwisho mwisho za upandaji wa ligi kuu inabidi tff waziangalie sana,Ila nashukuru Mungu katika kituo A huku dar mambo ni shwari kabisa
 
Kuna kipindi cha mpira kilikua kinonyeshwa itv miaka fulani kuna segment ilikua inaitwa African Magic, humo utaona magoli ya ajabu kabisa na kipa kuokoa kwa mtindo wa ajabu mno.
 
Back
Top Bottom