Kwa utafiti wangu mdogo niliofanya, ongezeko la vidonda vya tumbo na bawasiri husababishwa zaidi kwa kupuuza ama kula kidogo mboga za majani

Kwa utafiti wangu mdogo niliofanya, ongezeko la vidonda vya tumbo na bawasiri husababishwa zaidi kwa kupuuza ama kula kidogo mboga za majani

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Sikuhizi imekuwa kawaida sana watu kula ndizi, wali, ugali huku mboga ikiwa ni maharage, nyama, mchuzi, n.k. bila kutumia mboga za majani aina ya chakula maarufu chenye nyuzi kama figili, mchicha, n.k. kama ipo inakuwa ni kiasi kidogo sana ukila tonge mbili za kipimo sahihi habari imeisha.

Hapo zamani migahawa ilikuwa michache na watu wengi walikula nyumbani au kujipikia, urahisi wa bei za mboga za majani ulifanya tule ya kutosha bila kujibana bana, tonge moja unachota mboga ya kutosha sio kama sikuhuizi migahawani mboga ni ya kuila kwa hesabu.

Binafsi kuna kipindi niliwahi kuwa mhanga japo haikuwa serious, ugonjwa unakuja na kupotea na wala sikutumia dawa yoyote, nilichogundua ninavyopuuza mboga za majani ugonjwa unarudi, nikiongeza ulaji wa mboga za majani unapotea kabisa.

Mboga za majani ni vyakula vya nyuzi nyuzi na ni bei rahisi mno kuzidi matunda yenye nyuzi.

Nashauri wenye magonjwa haya ikibidi baadhi ya ratiba wawe wanakula mboga tu.
 
USIOMBE YAKUPATE, BORA VIDONDA VYA TUMBO KULIKO VIDONDA VYA UTOMBO, DEUDENUM URCERS.

UTATESEKA KAMA UMEROGWA, UTAONA KILA RANGI.

ACHANA NA HPYROLE KABISA
 
Chanzo kikuu cha ugonjwa wa vidonda vya tumbo (peptic ulcers) ni maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori na matumizi ya muda mrefu ya dawa za kupunguza maumivu, hasa za kundi la NSAIDs (Non-Steroidal Anti-Inflammatory Drugs) kama vile aspirin na ibuprofen.

Mambo mengine yanayoweza kuchangia ni pamoja na:

1. Uvutaji wa sigara: Unaweza kuongeza hatari ya vidonda vya tumbo kwa sababu huongeza uzalishaji wa asidi kwenye tumbo.

2. Unywaji pombe kupita kiasi.
Pombe inaweza kudhoofisha utando wa tumbo na kuongeza asidi ya tumbo.

3. Lishe isiyofaa Ingawa chakula kwa ujumla hakisababishi vidonda vya tumbo, vyakula vyenye viungo vikali au vyenye asidi nyingi vinaweza kuzidisha hali hiyo.

4. Msongo wa mawazo: Msongo wa mawazo unaweza kuzidisha dalili za vidonda vya tumbo lakini kwa kawaida si chanzo cha moja kwa moja.

Kwa ujumla, Helicobacter pylori na matumizi ya NSAIDs ndizo sababu kuu zinazojulikana za ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
 
Sikuhizi imekuwa kawaida sana watu kula ndizi, wali, ugali huku mboga ikiwa ni maharage, nyama, mchuzi, n.k. bila kutumia mboga za majani aina ya chakula maarufu chenye nyuzi kama figili, mchicha, n.k. kama ipo inakuwa ni kiasi kidogo sana ukila tonge mbili za kipimo sahihi habari imeisha.

Hapo zamani migahawa ilikuwa michache na watu wengi walikula nyumbani au kujipikia, urahisi wa bei za mboga za majani ulifanya tule ya kutosha bila kujibana bana, tonge moja unachota mboga ya kutosha sio kama sikuhuizi migahawani mboga ni ya kuila kwa hesabu.

Binafsi kuna kipindi niliwahi kuwa mhanga japo haikuwa serious, ugonjwa unakuja na kupotea na wala sikutumia dawa yoyote, nilichogundua ninavyopuuza mboga za majani ugonjwa unarudi, nikiongeza ulaji wa mboga za majani unapotea kabisa.

Mboga za majani ni vyakula vya nyuzi nyuzi na ni bei rahisi mno kuzidi matunda yenye nyuzi.

Nashauri wenye magonjwa haya ikibidi baadhi ya ratiba wawe wanakula mboga tu.
🌳 VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAKE🌳
⚡Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mfumo unaohusika na umeng'enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili.
⚡Sehemu kuu zinazohusika katika umeng'enyaji huo ni kinywa, umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach', ini, mfuko wa nyongo, utumbo mwembamba 'Duedenum & Ileum', kongosho, utumbo mpana na puru 'Rectum'.
⚡Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng'enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika kama 'Peptic ulcers'.

stomach_ulcers
Vidonda vya mfumo wa umeng'anyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita vidonda vya tumbo 'Gastric ulcer', vikiwa katika duodenum tunaita 'Duodenal ulcer' na vikiwa katika esophagus tunaita 'Esophageal ulcer'

☘SABABU ZA VIDONDA VYA TUMBO☘
👉Bakteria aina ya Helicobacter pylori 'H.pylori' & Non-Steroidal Anti Inflammatory Drugs 'NSAIDs' ndio visababishi vikuu.
👉Bakteria H.pylori wanahusika sana kwa angalau nne ya tano ya vidonda vya tumbo 'Gastric ulcers' & 95% ya 'Duodenal ulcers' ambapo NSAIDs husababisha 20% ya 'Gastric ulcers' na 5% ya 'Duodenal ulcers'
👉Bakteria H.pylori husababisha kupitia vyakula na maji. Pia hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo wakati mkila denda/kunyonyana midomo.
👉Bakteria H.pylori huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng'enya 'Enzyme' iitwayo 'Urease' inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo.
👉Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo.
👉Non-Steroidal Anti Inflammantory Drugs 'NSAIDs' ni dawa za kutuliza maumivu ya kichwa, maumivu ya hedhi, kushusha homa na kuondoa maumivu madogo madogo mfano Aspirin, Ibuprofen,Diclofenac & Meloxicam. Dawa hizi hupunguza uwezo wa kuta za tumbo na kufanya uwe rahisi kushambuliwa na asidi za tumboni hivyo kusababisha vidonda.
👉Chembe za urithi 'Genetics': Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya tumbo wana ndugu wa karibu wenye vidonda pia, hii huwafanya wataalamu kufikiria kuwa chembe za urithi zinahusika pia.
👉Uvutaji sigara/tumbaku: Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta.
👉Matumizi ya pombe/vilevi: Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo/pombe.
👉Msongo wa mawazo 'Mental stress': Msongo wa mawazo hausababishi vidonda moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa.

🌿DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO🌿
⚡ Maumivu ya tumbo na huwa makali zaidi pale asidi inapopita juu ya vidonda.
...Maumivu yanaweza anzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua 'Epigastric pain'
...Maumivu yanaweza kuongezeka unapokuwa njaa. Pia yanaweza kuwa makali wakati wa usiku kwenye mida ya kulala, yanayoweza kupunguzwa kwa kula chakula kidogo.
⚡ Kushindwa kumeza vizuri chakula.
⚡ Chakula kukwama kama kinataka kurudi mdomoni.
⚡ Kujisikia vibaya baada ya kula.
⚡ Kupungua uzito.
⚡ Kukosa hamu ya kula.

🌴DALILI HATARI🌴
⚡Kutapika damu.
⚡ Kupata choo kikubwa cheusi au chenye damu nzito.
⚡ Kichefuchefu & kutapika.

JINSI VIDONDA HUGUNDULIWA:-

Maelezo ya mgonjwa juu ya dalili alizonazo humsaidia daktari kuhisi kinachomsumbua mteja wake ni vidonda vya tumbo.

Ili kuthibitisha vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika :-

Kupima damu 'Blood test'

Kuangalia bakteria aina ya H.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibayotiki au dawa za vidonda Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi 'Negative'

Kupima pumzi 'Breath test'

Mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjika, hii hufanya bakteria H.pylori kuvunjika na baada ya lisaa mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa kama mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi.

Kupima antijeni kwenye kinyesi 'Stool antigen test'

Kipimo hiki huangalia kama kuna bakteria H.pylori kwenye kinyesi. Vilevule kipimo hiki hutumika kuangalia ufanisi wa matibabu yaliyotolewa dhidi ya bakteria.

X-ray ya sehemu ya juu ya tumbo 'Upper gastrointestinal x-ray'

Picha huonyesha umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach' na Dudenum. Mgonjwa humeza maji yenye 'Barium' ambayo hufanya vidonda kuonekana kirahisi kwa x-ray.

Kamera ya tumbo 'Endoscopy'. Mrija mrefu wenye kamera huingia tumboni na daktari huona vidonda kwenye skrini ya kompyuta 'Monitor'.

⚡MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO⚡
Kama vidonda vitakuwa vimesababishwa na bakteria H.pylori dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa.

Kama vidonda vya tumbo vitakuwa vimesababishwa na 'NSAIDs' na hana maambukizi ya bakteria H.pylori atapaswa kutumia dawa Proton Pump Inhibitors 'PPIs'

Proton Pump Inhibitors 'PPIs' hufanya kazi kwa kuvunja/kuzuia kazi ya protini ziitwazo 'Proton Pump' ambazo huhusika katika utengenezaji wa asidi tumboni.

Matumizi ya NSAIDs kwa ajili ya kuondoa homa na maumivu yatalithiwa na dawa kama Paracetamol.

Matibabu yaliyozungumziwa hapo juu yanaweza kuchukua muda kabla ya kuanza kufanya kazi hivyo daktari anaweza kuongeza matibabu mengine kama vizuia asidi 'Antiacids' & 'Alginates' kwa ajili ya nafuu ya haraka.

Usitumie dawa hizi ndani ya lisaa moja baada ya kunywa PPIs mfano Omeprazole au H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine.

⚡⚡Matibabu kwa njia za asili, zipo dawa mbali mbali unazoweza tumia zikiwa kwenye mfumo wa unga au kimiminika

~CHIEF SANG'IDA
 
Sikuhizi imekuwa kawaida sana watu kula ndizi, wali, ugali huku mboga ikiwa ni maharage, nyama, mchuzi, n.k. bila kutumia mboga za majani aina ya chakula maarufu chenye nyuzi kama figili, mchicha, n.k. kama ipo inakuwa ni kiasi kidogo sana ukila tonge mbili za kipimo sahihi habari imeisha.

Hapo zamani migahawa ilikuwa michache na watu wengi walikula nyumbani au kujipikia, urahisi wa bei za mboga za majani ulifanya tule ya kutosha bila kujibana bana, tonge moja unachota mboga ya kutosha sio kama sikuhuizi migahawani mboga ni ya kuila kwa hesabu.

Binafsi kuna kipindi niliwahi kuwa mhanga japo haikuwa serious, ugonjwa unakuja na kupotea na wala sikutumia dawa yoyote, nilichogundua ninavyopuuza mboga za majani ugonjwa unarudi, nikiongeza ulaji wa mboga za majani unapotea kabisa.

Mboga za majani ni vyakula vya nyuzi nyuzi na ni bei rahisi mno kuzidi matunda yenye nyuzi.

Nashauri wenye magonjwa haya ikibidi baadhi ya ratiba wawe wanakula mboga tu.
🍀 BAWASIRI/MGOLO 🍀
⚡Bawasiri ni ugonjwa unaotokea katika njia ya haja kubwa, hujitokeza kama uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje.
⚡Kwa kiingereza hujuliakana kama piles.
⚡ Na kitaalam hujulikana kama hemorrhoids

🍃AINA ZA BAWASIRI🍃
👉1⃣ BAWASIRI YA NJE
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina hii ya bawasiri kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
👉2⃣BAWASIRI YA NDANI
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu.
⚡Aina hii imeainishwa katika mainisho ya madaraja manne yafuatayo:
👉Daraja la 1 - Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
👉Daraja la 2 - Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya haja.
👉Daraja la 3 - Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya haja.
👉Daraja la 4 - Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya haja.
+255 656 303 019
🌱BAWASIRI HUSABABISHWA NA NINI?🌱
👉Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu
👉Ujauzito – wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa
👉Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile
👉Uzee – kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu
👉Sababu za kurithi – baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni asilimia ndogo sana.
👉Kuharisha sana kwa muda mrefu
👉Kutumia vyoo vya kukaa
👉Kunyanyua vyuma vizito
👉Mfadhaiko/stress
👉Uzito na unene kupita kiasi.

🌱DALILI ZA BAWASIRI🌱
👉Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
👉Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia
👉Muwasho sehemu ya tundu la haja kubwa
👉Uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa
👉Haja kubwa yaweza kujitokea tu muda wowote

🌿ATHARI ZA BAWASIRI🌿
⚡ Upungufu wa damu mwilini
⚡ Kutokwa na kinyesi bila kijitambua
⚡Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa
⚡Kupungukia nguvu za kiume (kwa wanaume)
⚡Kupungukiwa na uwezo wa kufanya kazi kutokana na maumivu
⚡Kupata tatizo la kisaikolojia

🌿NJIA ZA KUJIKINGA DHIDI YA BAWASIRI🌿
⚡Kula mboga za majani na nafaka zisizo kobolewa kwa wingi
⚡Kunywa maji mengi lita sita hadi kumi na mbili kwa siku
⚡ Acha kufanya ngono kwa kutumia tundu la haja kubwa (kulawitiwa)
⚡ Punguza kukaa chooni kwa muda mrefu, kunaweza kuongeza shinikizo katika njia ya haja kubwa.

Kwa ushauri na dawa za magonjwa mbalimbali wasiliana nami
+255656303019
~Chief Sang'ida.
 
Back
Top Bottom