makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Kama kuna kitu ambacho kimenikera na kunikarihisha ni uteuzi wa majina 201 uliofanywa na Rais Kiwete kwa Wabunge watakaoingia kwenye Bunge la Katiba mpya wiki ijayo.
Hakuna aliyetarajia kukutana na orodha hii ndefu ya Makada wa CCM wakipewa ulaji wa kuingia kwenye Bunge hili litakalohitimisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya ambayo haitakuwepo labda utokee muujiza wa Mungu. CCM wamesha apa bila Serikali 2 hakuna Katiba mpya na tutaendelea na Katiba ya zamani kwa manufaa ya CCM!!!
Kwa uteuzi huu Raisi kiwete amedhihirisha nia ya Chama chake cha CCM na yeye mwenyewe ya kutokuwa tayari kuwapa Watanzania Katiba mpya baada ya miaka 50!. Itakumbukwa kwamba wazo la Katiba Mpya lilikuwa wazo la kutoka upinzani hasa CHADEMA wakti wa kampeni na baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010. CCM hata siku moja kabla na baada ya hapo hawakuwahi kutamka juu ya swala hili nyeti la kutaka kuwapa Watanzania Katiba mpya.Swala la Katiba Mpya halijawahi kuwa kwenye ILANI wala SERA za CCM tangu mwaka 1961 enzi za TANU!
Kwa vile Rais Kiwete ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa CCM hana mpango wowote wa Katiba Mpya, alichoamua kufanya Kiwete na CCM yake ni kucheza na akili za Watanzania kwa kuigiza the Comedy Show ya Katiba mpya ambayo ni kiini macho na haitakuwepo! Nitaeleza. CCM wamecheza na Sheria,kanuni, na taratibu za Bunge la Katiba kwa kuhakikisha kuwa Rais Kiwete akisaidiana na Rais wa BMZ ndiyo waliopewa mamlaka makubwa ya kuweza kuchagua na kuteua WATU NA MAKADA WAO WA CCM WANAOWATAKA pasi na kuhojiwa na yeyote! Hii maana yake ni kujihakikishia ushindi kwa kuweka uwiano ambao piga ua maamuzi yoyote ya KURA ndani ya Bunge hili yatawapa USHINDI CCM!
Tunajua Bunge la Tanzania lina Wabunge zaidi ya 350 ambao wanaingia moja kwa moja, kati ya hawa zaidi ya 75% ni Wabunge wa CCM (250+). Hii tayari ni zaidi ya 2/3(theluthi 2) ya kura zinazotakiwa kupigwa kutetea hoja yoyote ndani ya Bunge la Katiba. Ili kukoleza hii hesabu ya 2/3 Rais Kiwete akaamua kuongeza Makada wengine kwenye hesabu hii ya 201.Uchambuzi wa kina unaonyesha zaidi ya 80% ni Makada au Wana CCM! Wapo waliovaa majoho ya vyama uchwara vya Upinzani ilhali ni CCM damu! Ukiangalia hii orodha imejaa udanganyifu mkubwa. Kuna watu kama kizee Kingunge Ngombale Mwiru kuingia kwenye Bunge hili eti kama mjumbe toka NGO ni kichekesho!!Tangu lini CCM ikawa NGO???Kila mtanzania anajua Kingunge ni nani ndani ya nchi hii na anafanya nini??? Leo kuwalaghai Watanzania kuwa huyu ni kizee aliyechoka na mwenye mawazo mgando ni mwana NGO! Tayari Kingunge ameshaweka msimamo wake wa SERA YA CCM na Serikali 2 na ndiyo anayoingia nayo kule Bunge la Katiba!!!What a shame???
Kitakachofanyika kwenye Bunge hili la Katiba ni kutetea hoja za CCM kwa nguvu zote mwanzo hadi mwisho. Tayari Kiwete ameshabainisha kuwa SERA YA CCM NI SERIKALI 2 na si vinginevo na ndiyo itakayopigiwa debe na kupitishwa kwa kura zaidi ya 2/3! Tume ya Warioba kwenye Rasimu #1  Watanzania zaidi ya 62% WAMEPENDEKEZA SERIKALI 3 lakini CCM hawataki! Hata kama Wananchi kwenye kura ya MAONI watataa serikali 2 maana yake ni kwamba TUTARUDI kwenye KATIBA YA ZAMANI kama alivyowahi kuonya Rais Kiwete! Hilo ndiyo lengo na ndiyo mkakati wa CCM utakaokwenda kuungwa mkono na Wabunge wa CCM ambao ni zaidi ya 2/3!!!
Nawapa pole sana Watanzania kwa kunyima haki yao ya kuchagua KATIBA MPYA wanayoipenda. Kwa mara nyingine tena CCM wameweza kudhihirisha UMWAMBA wao kwenye DEMOKRASIA ya kuchagua. Umwamba ambao aghalabu wamekuwa wakiutumia hata kwenye Chaguzi ndogo na Kuu za katika nji hii ili kupata Ushindi ambao wao hudai ni wa KISHINDO!!!!
Tubiri.