Kwa uwanja huu wa Mkwakwani ulivyo na umetoka kwenye matengenezo hii bodi ya ligi mjiuzilu tu

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
62,101
Reaction score
38,487
Wapendwa ktk bwana

Nawasalimu kwa heshima ya jamhuri ya muungano wa tanzania

Wakati sisi simba lialia tunaendelea kulalamikia tuchexe final kwa mkapa


Na huku caf wakilalamika uwanja haujakidhi

Na

Final n Zanzibar

Sasa ukisubiria vichekecho vya caf kurudisha mechi kwa mkapa

Nani alieangalia mechi ya yanga mkwakwani

Hivi mnajua huu uwanja ulifungiwa na tff mda coastal union akaenda kucheza arusha sheikh amri abeid karume

Hawa hawa wakaenda kuangalia marekebisho wakarudisha mechi zote za coastal tanga means umefunguliwa rasmi

Wapendwa hii n nchi yetu sote tusikubali wachache kutumia kama shamba la bibi

Hii mechi ya yanga mvua imemwagika kidogo tu gafla uwanja sio uwanja tena

Nashauri wizara husika tuchunguze viwanja vyote...haiwezekani huu uwanja unahifadhi

Maji hivi na hata nusu mwaka haijafika imetoka kufanyiwa marekebisho na kufunguliwa

Ikiwezekana tuagize watu toka nje wakague viwanja vyetu waseme vipi vinaweza kuendelea kuchezwa

Else tunawaumiza hawa wachezaji wetu wapendwa nao n binadamu

Bodi ya ligi

Ushauri wa bure tu mjiuzilu

Maana kama viwanja tu vimekuwa shida kuvisimamia vipi mambo mengine

Mungu Ibariki Tanzania

Your browser is not able to display this video.
 
Serikali inapambana kupaka rangi yenye bendera ya taifa majukwaani si katika pitch, tayari tumefanya hivyo uwanja wa mkapa na mkwakwani bado ccm kirumba,A.H.MWINYI na ccm sokoine mbeya, watanzania niwape moyo,endeleeni kukamuliwa kodi kwa ajiri ya maboresho ya majukwaa na upakaji wa rangi. Kama hamtaki tutawalazimisha mhamie Burundi.
 
Rais anabung'aaa bung'aa tu watu wanapiga hela,Marekebisho ya kwa mkapa yaliyofanyika hayazidi Billion 15,watu wameshasepa na kibunda aisee

Hapo Mkwakwani nilijua kutakuwa na maajabu,kumbe wameishia kupaka rangi majukwaa tu ukarabat wa mwaka mzima
 
Ccm Kirumba imeshapakwa marangi ya Bendera ya taifa,Sokoine tayari,Jamhuri Dodoma tyr,Jamhuri Morogoro Tayari sijui nani alikuja na ubunifu huu..Hivi unajua kwamba bei ya stadium seat kwa piece moja china huwa ni dola 5? Na zinauzwa peace kuanzia 1000 .Let say serikali imeagiza viti china tuseme seat zote za Benjamin Mkapa 60000 kwa bei ya dola 5 kwa piece moja,hapa itakuwa imetumika dola 300,000 tu ambayo ni TZS 810,000,000 lakini wajanja wamepewa Billion 30 wameishia kuweka viti vipya tu pale kwa Mkapa.Pesa iliyotumika pale hata Billion 10 haifiki
 
Unaowaambia wafuatilie ndio wapigaji wenyewe. Ulaji wa watu huo, shamba la bibi. Uzuri vita dhidi ya ufisadi sio shida zake. "Kula kwa urefu wa kamba".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…