MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nimepokea messages nyingi sana toka kwa wanaJF wengi kutaka kujua maoni yangu kuhusu suala la Diddy kwasababu mimi ni shabiki mkubwa wa muziki wa Hiphop na mtu mwenye akili mingi. Nilikuwa sitaki kuongelea hili jambo ila nimeona niongelee muziki kwa ujumla jinsi ulivyo katika ulimwengu wa leo. Ingawa sijaona uzi wa Lucas Mwashambwa akizungumzia hizi ishu ila watu wengi wameandika mitandaoni ikiwemo JF.
Muziki sio jambo baya kwasababu hata kwa sisi wakristo tumeona muziki ukitajwa kwenye biblia. Mfalme Daudi alikuwa mwanamuziki professional mwenye kipaji. Tatizo ni kuwa shetani naye kama kiumbe smart sana huwa anawekeza kwenye mambo yanayopendwa na binadamu ili kupata wafuasi wengi. Muziki na mavazi ni mambo ambayo shetani kafanya uwekezaji mkubwa mno unaomletea mafanikio kila kukicha. Tuhuma alizo nazo Diddy sio za bahati mbaya. Zimeanzia kwenye muziki hadi kwenye mambo hizo tuhuma.
Miziki ya aina zote hadi huu wa injili una mkono wa shetani. Angalia idadi ya ndoa za wanamuziki wa injili zilizovunjika baada ya kuingia kwenye muziki utapata jibu sahihi. Hata kwenye kundi ninalolipenda la Zabron Singers kuna kashfa mbaya ya binti kujiengua kwenye kundi kisa kikitajwa ni kukosana na hawara yake aliye naye kundini. Yaani ushenzi mtupu. Kwenye kwaya makanisani nako kuna kashfa za watu kupelekeana moto. Yaani muziki kwa ujumla una ushetani ndani yake.
Ikumbukwe muziki ndo kazi ya halali yenye pesa nyingi zaidi kwahiyo ni ngumu mno kwa wanamuziki kukwepa mitego ya shetani aliyoiweka kwenye muziki. Kuhusu Diddy tusubiri hukumu ya mahakama. Kwa sasa hana hatia hadi mahakama itakapothibitisha tuhuma zake.