Kwa vijana wote ambao upande wao vimekaza

miamiatz

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
505
Reaction score
941
Kwanza tutoke mafichoni. Tujitokeze mitaani kuangalia je ni fursa gani zipo. Makala iliyopita nilitoa mfano wa makala ya muuza matunda. Leo naomba nitoe makala nyingine inayofanania.

Kuna rafiki yangu anaishi msata na anajishuhulisha na ufugaji wa ng'ombe wa maziwa. Kuna kijana mmoja alikuwa akisomea masuala ya business administration chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 2013. Yule kijana alikuwa akijaribu kutoka hostel siku za wikiendi na kutembelea maeneo mbalimbali ya mkoa wa pwani.

Katika pitapita yake hakuwahi kuwaambia watu kuwa yeye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam. Katika pitapita hizo akafanikiwa kukutana na yule rafiki yangu anaejishuhulisha na ufugaji wa ng'ombe wa maziwa. Kijana alikuwa muongeaji mzuri na mstaarabu.

Waliongea mengi ila hakumwambia kuwa ni mwanafunzai wa chuo kikuu cha Dar es Salaam anaekaribia kuhitimu.

Alipohitimu alirudi msata kwa yule rafiki yangu. Akamwambia katika pita pita yake ya kutafuta maisha ameona bora aje pale yupo tayari kuajiriwa hata kwa kujitolea ilimradi apate pa kulala pale nyumbani kwa rafiki yangu na huduma za lazima kama chakula, matibabu, etc kama mmoja wa wanafamilia.

Kwakuwa kijana alionekana mstaarabu sana basi alipokelewa. Walifanya wote kazi za pale kwa miezi mitatu na yule rafiki yangu akaona kijana ana upeo mkubwa sana. Akaanza kumdadisi ila kijana hakujielezea elimu yake ya juu alieleza kuwa aliishia darasa la saba.

Huyo rafiki yangu akawa akimtegemea sana yule kijana kusimamia mradi mzima na kijana alikuwa muaminifu sana mpaka ikafika wakati akaanza kulipwa laki3 kwa mwezi.

Yule kijana kwao ni morogoro. Alipopokea kwa miezi sita akaomba akasalimie wazazi. Alipoenda akajenga banda la kutosha ng'ombe kumi wa maziwa kwa kutumia ile 1.8m aloipata.

Akarudi kazini na kuendelea na kazi. Yule rafiki yangu alikuwa pia akiuza ndama mara kwa mara. Kijana alikuwa ndio mtafutaji wateja. Akaanza kununua mmoja mmoja kila mwezi. Ndama mmoja aliuzwa 250,000 na alikuwa akishanunua anatumia 50,000 kumfikisha kwao morogoro.

Baada ya miezi mitano alikuwa na ndama watano kwenye lile banda kule morogoro ambao walikuwa wakihudumiwa na mama yake mzazi kwa pumba na mabua ya mahindi na majani. Mama alipokuwa na pesa kidogo alinunua viambata muhimu madukani kwa ajili ya chakula cha ndama.

Kijana aliukuza mradi wa rafiki yangu ukawa mkubwa kwa miaka mitatu huku nae akiwa na jumla ya ng'ombe 10 kule morogoro wakihudumiwa na mama yake.

Kijana saivi, miaka mitano baada ya kuhitimu, anaendesha miradi miwili, ule wa morogoro na ule wa msata. Wa morogoro ana ng'ombe 15 kwa sasa na kwa wastani anapata lita 200 za maziwa kila siku kule morogoro. Nusu ya mapato yote hurudi kwenye garama za uendeshaji na hubakiwa na pesa ya lita 100 ambayo kwa bei ya 1,000 kwa morogoro hujipatia 100,000 kila siku faida.

Mpango wake ni kuwa na ng'ombe 100 baada ya miaka mitano. Sasa wewe uking'ang'ana na mavyeti na kujibusti utachelewa basi na treni pia litakuacha. Kumbuka safari ya kutembea kwa miguu ni nzito sana usikubali kuachwa na basi na treni pia.
 

Attachments

  • IMG_20180417_101923_533.jpg
    92.1 KB · Views: 63
Safi sana mkuu nimekuelewa
 
nzuri ngoja niuze ka s8 plus nianze ujenzi wa banda nikimaliza ujenzi nauza laptop nanunua ndama wawili kwa ajiri ya kuanzia mradi
 
nzuri ngoja niuze ka s8 plus nianze ujenzi wa banda nikimaliza ujenzi nauza laptop nanunua ndama wawili kwa ajiri ya kuanzia mradi
Usipokuwa na simu janja (smart phone) mijadala ya JF itakupita
 
nzuri ngoja niuze ka s8 plus nianze ujenzi wa banda nikimaliza ujenzi nauza laptop nanunua ndama wawili kwa ajiri ya kuanzia mradi
Ha ha yule aliyeuliza kule ''sasa wote tukauze matunda?" yupo wapi aje aulize na hapa sasa wote tukafuge ng'ombe wa maziwa?πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…