Kwa wabunifu na wadau wa ubunifu: Hudhuria wiki ya ubunifu katika mkoa wako

Izzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
553
Reaction score
1,144
Habari wana Jukwaa,

Sambamba na UZI HUU niliouleta kuhusu Wiki ya Ubunifu Mkoa wa Njombe, nimeona ni vyema nikaleta masasisho kuhusu matukio kuelekea Wiki ya Ubunifu kitaifa itakayofanyika Dodoma. Hapa nawaletea orodha ya Mikoa ambako kuna matukio yatafanyika, Taasisi zinazohusika kuyaandaa na Tarehe. Ikiwa unahitaji kushiriki basi wasiliana na Taasisi husika, ikiwa mawasiliano ni changamoto, naweza kukuunganisha nao - nina mawasiliano ya wote.

Yote haya yanafanyika kwa imani moja kubwa: Kwamba UBUNIFU utatusaidia kuyafikia maendeleo kwa haraka na kwa ufanisi zaidi.
NB: Kuna mikoa tayari wameshafanya.

1. ARUSHA: Westerwelle Foundation Tanzania - Tarehe 9 - 13 Mei, 2022.
2. DODOMA: Capital Space Limited - Tarehe 15 - 20 Mei, 2022.
3. IRINGA: R-Labs - Tarehe 12 - 14 Mei, 2022.
4. MBEYA: MUST - Tarehe 9 - 13 Mei, 2022.
5. ZANZIBAR: Cube Zanzibar - Tarehe 10 - 14 Mei, 2022.
6. MTWARA: SIDO - Tarehe 13 Mei, 2022.
7. MWANZA: SIDO - Tarehe 25 - 29 Aprili, 2022
8. TANGA: Projekt Inspire Ltd - Tarehe 6 Mei, 2022.
9. MOROGORO: The Arena of Taking Charge (TAOTIC) - Tarehe 6 - 13 Mei, 2022.
10. NJOMBE: Valiant Hands of Care (VAHACA) Foundation - Tarehe 11 - 13 Mei, 2022.
11. KILIMANJARO: Kilistart - Tarehe 6 - 7 Mei, 2022.
12. KAGERA: KADETFU - Tarehe 27 - 30 Aprili 2022.
13. KIGOMA: SIDO - Tarehe 9 Mei, 2022.
14. MARA: Buhare CDTI - Tarehe 9 Mei, 2022.
15. RUVUMA: Mlale Digital Innovation Centre - Tarehe 6 Mei, 2022.
16. DAR ES SALAAM: TAI Volunteers - Tarehe 9 - 12 Mei, 2022.

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti hii: INNOVATION WEEK TANZANIA





















 
Hizo tarehe ziko sawa kweli hususani miezi..mana kuna mikoa mingine muda ushapita..sasa mbona kuleta taarifa hii kwa mikoa ambayo muda umepita.?

#MaendeleoHayanaChama
 
Mbona mikoa mingine haipo?
Ndio, haifanyiki mikoa yote - ni kwa mikoa 16 tu ambayo ina Taasisi zinazofanya kazi aidha na COSTECH au na UNDP kupitia programu yao ya FUNGUO. Watazidi kuongeza mikoa mingine kadiri muda unavyoenda (Mwakani na kuendelea)
 
Hizo tarehe ziko sawa kweli hususani miezi..mana kuna mikoa mingine muda ushapita..sasa mbona kuleta taarifa hii kwa mikoa ambayo muda umepita.?

#MaendeleoHayanaChama
Tarehe ziko sahihi kabisa. Mipango ya Wiki ya ubunifu ilianza tangu mwishoni mwa mwaka jana. Lakini kwasababu ya masuala ya itifaki na michakato ya Serikali, orodha hii ya mikoa, taasisi na tarehe imechelewa kuthibitishwa na Wizara kupitia COSTECH, na ndio maana mimi nimeileta wakati wengine wameshafanya. Naamini hutashangaa, ndivyo mifumo yetu ilivyo... taratibu sana.

Nilikuwa nasubiri uthibitisho kutoka COSTECH, kwasababu wengi wao wamebadilisha tarehe za matukio ikiwemo Njombe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…