Kwa Wadada Wanaotaka Kuolewa

Kwa Wadada Wanaotaka Kuolewa

Sisa Og

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2024
Posts
201
Reaction score
504
Habari wana JF?

Leo nazungumza na wadada wanaotamani kuolewa. Kumiliki mwanaume. Kama hauna mpango huo, basi endelea na threads nyingine.

Haijalishi mdada ni mrembo kiasi gani, una tabia nzuri kiasi gani. Ila hizi tabia zitakufanya uishie kuwa single mother, uchukie wanaume au wakufaidi wastaafu. Tabia hizi zinafukuza wanaume wa aina hii
  • Wanaojielewa
  • Wanaoelewa/wazoefu wa mapenzi
  • Walio serious na wewe na
  • Wenye washauri ( Wale wenye kupokea ushauri from different elders or experts)

Na hizo tabia watazivumilia wanaume wa aina hii:
  • Nice Men
  • Waliolelewa na single mother ( mnisamehe)
  • Wasiojielewa/uzoefu katika mapenzi

TABIA NI HIZI HAPA:
* Kuomba Hela
Kama unataka uishie kuchukuliwa kama cheap, ambitious, drama queen n.k. endelea kuomba omba pesa kwa kila mwanaume anayekuja maishani mwako. Kwa sasa utaona unafaidi ila siku moja utamtafuta wa kukupa hela na hutomuona.
Ni hivi, Kila mwanaume anapotaka kuoa, kigezo cha kuomba hela kinakuwa kwenye orodha. Haijalishi anazo au hana. Ndo maana matajiri wanatenga hadi hela za kuonga. Hao washaoa na hawana hasara wanachotaka ni burudani ila muoaji anahitaji heshima, uvumilivu na maelewano wewe so bidhaa. NB: Wanaume tunaambizana sababu za kuachana na nyie. John akisikia Juma ameachana na Anna sababu ya hela, basi John anatenga 100k ya kutumia kama chambo ili kumpata Anna. Hela ni sehem ya udhaifu. Mwanaume anaogopa na kumuheshimu mwanamke anayekataa mitego ya pesa. Kama udhaifu wa dem ni pesa, mwamba atatoa mpaka laki kadhaa ili apewe hata Yas na kwakuwa dem amewekeza akili yake huko basii imeisha hiyo.
Simanishi usiombe hela ila kuna uombaji ni balaa.

*Kumjaribu Mwanaume
Dada, wanaume tuna mambo mengi. Na hatupendi kudharauliwa au kutothaminiwa. Ndo maana hata shuleni ugomvi wa wa darasani mara nyingi ni wavulana.
Akija mkaka wa watu ukaanza kumletea nyodo, unataka yeye ndo akutetemekee wewe ni mzee wa kureply. Simu hupigi, SMS unajibu kwa masaa, short and clear. Mara unampanga. In short wazungu wanasema playing hard to get. Basi hapo sisi wanaume tunajikataa. Ndo utasikia siku hizi wanaume hawabembelezi. Usitumie njia alizotumia mama yako kumtega baba yako miaka ya 70's. Njia ya kumtega mwanaume ni moja tu, muoneshe pande zako mbili (hasi na chanya) mapema ili akae akijua jinsi ya kukabiliana na wewe mapema. Kama unakula nusu ya wali usiiigize kula robo. Hutoigiza mwaka mzima acha maigizo. Wanaume wa kuvumilia hiyo michezo wapo ndo nice men. Na uzuri mnaishiaga kuwaliza sababu hao sio wanaume halisi.

Nimemaliza. Asante kwa kusoma.
 
Yaani vitoto vya afumbili vinaomba hela hivyooo 🤣🤣🤣

Unakuta msichana yuko 30+ na yeye anajifanya bado yumo wakati jua linaelekea kuzama.

Wasichana/Wanawake ushauri huu uzingatieni sana
 
Hapo point yako kuu “Kuombwa pesa” 😹😹
Nasemaje PESA utaombwa iwe unataka kuoa au kupita, hiyo haituhusu.!! Tafuta pesa kijana/baba/mzee 🤣🤣
 
Yaani vitoto vya afumbili vinaomba hela hivyooo 🤣🤣🤣

Unakuta msichana yuko 30+ na yeye anajifanya bado yumo wakati jua linaelekea kuzama.

Wasichana/Wanawake ushauri huu uzingatieni sana
HATUTAKI 😹😹
 
Mmmh kwa tabia hizo mimi nakukimbia ndugu, hata wanaume wengine wanaojielewa watakukimbia Lamomy
Unakuwa sio muoaji, sasa km unakimbia kipindi cha uchumba kwenye ndoa mpk kifo utaweza kuhudumia??
 
Unakuwa sio muoaji, sasa km unakimbia kipindi cha uchumba kwenye ndoa mpk kifo utaweza kuhudumia??
Ninaweza kuwa na nia nzuri ya kukuoa ila ukanikimbiza kwa mizinga mmoja tu, kwa dunia ya sasa upate mwanaume umuombe hela kila mara halafu abaki na wewe, huyo atakuwa hana uzoefu na wadada. Wanaume wengi siku hizi wajanja, tunajua kuwa nyie wanawake kuna wanaume mnawapa papuchi bure bila kuwaomba hela

Wanaume wengi siku hizi, kwenye mwanzo wa mahusiano ukimuomba hata tsh elf 2, hata ukimuomba ukiwa na nia njema, alarm ya hatari ishalia kichwani kwake

Kuna Uzi miss natafuta aliuanzishaga, alilalamika mwanaume anakutongoza, ukimuomba hela anasitisha urafiki na anaacha kutongoza Lamomy
 
Km hujampenda na pesa huna ni sawa.

Wewe tatizo ushazoea kubeba mikasongo ya riverside, huku kwa wapenzi huwezi kupaelewa Balq 😹😹
 
Natumaini hauko serious. Just a joke
Hapo point yako kuu “Kuombwa pesa” 😹😹
Nasemaje PESA utaombwa iwe unataka kuoa au kupita, hiyo haituhusu.!! Tafuta pesa kijana/baba/mzee 🤣🤣
 
Back
Top Bottom