Dunia ina changamoto nyingi sana sio kwa wanawake tu bali hata wanaume japo wanaume hawa semi yanayo wakuta hadharani. Nakubaliana na ushauri wako japo unaweza kuwasaidia zaidi wanawake ambao walio na elimu na wenye uwezo wa kusimamia maisha yao bila utegemezi. Sehemu kubwa ya wanawake katika jamii yetu wameathiriwa na mfumo dume ambapo sehemu kubwa ya uchumi unamilikiwa na wanaume. Kutokana na mfumo huo sehemu ndogo ya wanawake wamebahatika kupata elimu nzuri na kumiliki uchumi na hawa kwa kiasi kikubwa wanapatika mijini. Baadhi ya wanaume katika jamii wanatumia matatizo ya kiuchumi na ya kijamii kuwadanganya wanawake kwa kutumia kigezo cha mahusiano na ahadi hewa lakini hawawahitaji kwa malengo yenye manufaa. Elimu ndio ukombozi wa wanawake katika nyanja zote kimapenzi na kiuchumi, hata mataifa yaliyoendelea wanawake wanathaminiwa kwa sababu wanamiliki uchumi na sio tegemezi kwa jamii ya wanaume hivyo anakuwa na nguvu ya kufanya maamuzi anayo yaona yeye ni sahihi katika maisha yake.