Kyenju
JF-Expert Member
- Jun 16, 2012
- 4,632
- 1,773
Juzi lafiki yangu alitumia tiba mbadala ili kutibu matatizo ya tumbo, baadaye kilichompata ilibidi tumkimbizie hospitalini.
Rafiki yangu huyo alitumia juice ya ukwaju ambapo alichanganya kiasi fulani cha ukwaju kwenye maji lita moja, nilimuuliza nani alimfundisha hii tiba akaniambia amejifunza kutoka kwa dr. bingwa wa tiba mbadala kupitia star TV.
Nilipo muuliza kuhusu ratio yaani mchanganyo anachanganya na ukwaju kiasi gani aliniambia kuwa kiasi cha ukwaju hakumbuki ila anakumbuka maji ni lita moja, dakika kama 20 baada ya kunywa juice ile alianza kukosa nguvu miguu ikalegea, akatokwa na jasho jingi mwili mzima ikabidi apelekwe chumba cha mapumziko maana tulikuwa kazini.
Jioni alirudishwa nyumbani lakini usiku hali ilikuwa mbaya maana alialisha sana kiasi cha kutokea hali fulani ya damu damu, kesho yake yaani jana ilibidi tumpeleke hospitali kwasasa amelazwa hospitali yuko kwenye dose.
Dr. alisema kuwa tatizo ni ukwaju ulikuwa mwingi sana kuliko maji ambapo umetengeneza acid tumboni.