Kwa wadau, wanaisimu na wajuzi waliobobea kwenye Kiswahili

che wa Tz

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2011
Posts
277
Reaction score
71
Hili ni swali wadau ambalo rafiki yake wa karibu kaniomba niliwakilishe kwa wanajamiiforum ili apate kujuzwa zaidi
"katika uchanganuzi wa sentensi za kiswahili, sentensi zilizooeleka zaidi na ambazo hutumika ni sahili, changamano na ambatano. Kwanini huwa hakuna uchanganuzi wa sentensi shurutia katika kiswahili"
 
Kwa Sababu Ni Sentensi Ambazo Ni Tegemezi Au Za Hali Fulani, kutokea Kwake Hutegemeana Na Masharti, hivyo Kuichanganua Ni Vigumu, kwa kuwa haichukui Viambajengo Muhimu Vya Uchanganuzi
 
Hili ni swali wadau ambalo rafiki yake wa karibu kaniomba niliwakilishe kwa wanajamiiforum ili apate kujuzwa zaidi
"katika uchanganuzi wa sentensi za kiswahili, sentensi zilizooeleka zaidi na ambazo hutumika ni sahili, changamano na ambatano. Kwanini huwa hakuna uchanganuzi wa sentensi shurutia katika kiswahili"

sentensi shurutia ni ya kisemantiki (sarufi maana) na ktk uchanguzi wa sentensi hatuhangaikii kinachomaanishwa bali muundo wa sentensi au mpangilio wa viambajengo vyake (sintaksia) hivo sentensi zenye muundo kamili ni sahili,changamano na ambatano ndizo huweza kuchanganuliwa (kimuundo)
 
Swali zuri, majibu mazuri.
Nami nimefaidika hapa
 
Hili ni swali wadau ambalo rafiki yake wa karibu kaniomba niliwakilishe kwa wanajamiiforum ili apate kujuzwa zaidi
"katika uchanganuzi wa sentensi za kiswahili, sentensi zilizooeleka zaidi na ambazo hutumika ni sahili, changamano na ambatano. Kwanini huwa hakuna uchanganuzi wa sentensi shurutia katika kiswahili"
Sentensi shurutia ni aina ya sentensi kwa mtazamo wa kidhima, na sentensi sahili, changamano na ambatano hizi ni sentensi zilizoainishwa kwa mtazamo wa kimuundo. Na kwa hiyo unapokuja katika uchanganuzi wa sentensi utaishia kuchanganua hizo tatu kwani wana muundo wao hawaitambui sentensi shurutia kama aina moja wapo ya sentensi.
 
Back
Top Bottom