Kwa wafanyabiashara tu. Tujadili jinsi ya kudeal na wachina ili usilizwe

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
27,031
Reaction score
49,928
Wale tunaodanga na bidhaa za wachina ili tupumue mjini na wale ambao mnataka kufanya biashara naomba tushauriane hapa ili kuepuka kulizwa na wachina jueni hakuna hela rahisi mjini

Maoni yangu Mimi wengine mtajazia usikubali kufanya mkataba na mchina eti anakufanya agent au distributor wa product yake eneo flani.mchina haaminiki akienda mtu mwingine na hela nae anampa mkataba mbaya zaidi na yeye anaingia soko hilo hilo kusambaza hyo bidhaa tena anashusha bei kumbuka yeye anatoka kiwandani .na mbaaaya zaidi hyo product anaweza kuitengenezea fake yake akauza tena cheap zaidi. Sasa hapo mzigo utakudodea na utaona bishara ovyo

Mzungu mzungu tu yeye akikupa kazi ya kudeal na eneo flani ni ngumu kupokea tena offer ya mtu mwingine kwa eneo hilo

Nimeona niseme hili na tushaurine maana naona watu wanagombana sana huko kimenuka. mchina kakaa pembeni naona anawacheka
 
Tunatakiwa tuhame kwenye kununua na kuuza, tuhamie kwenye kutengeneza na kuuza.
 
Ingia mkataba wa kisheria, kuwe na vipengele vya kumkamua fidia akikiuka masharti ya mkataba
 
Tunatakiwa tuhame kwenye kununua na kuuza, tuhamie kwenye kutengeneza na kuuza.
Hata kama unafanya hivyo kama unadeal na mchina hali ni hiyo hiyo.

tana kusuply mchina ni wa hovyo kabisa , kila siku anatafuta supplier wapya , hupangi jambo likapangika sababu kila siku rate imebadilika kutokana na supplier mtakavyokuwa wengi
 
Ingia mkataba wa kisheria, kuwe na vipengele vya kumkamua fidia akikiuka masharti ya mkataba
Wajanja mkataba ukiwa tight sana jua na kazi yenyewe hupati, kwanza hata huo mkataba mbovu wenyewe hadi mchina atoe jua unafanya kazi, maranyingi wanataka mkataba hewa
 
Wajanja mkataba ukiwa tight sana jua na kazi yenyewe hupati, kwanza hata huo mkataba mbovu wenyewe hadi mchina atoe jua unafanya kazi, maranyingi wanataka mkataba hewa
Teh teh teh... Akilazimisha na ukakubali kuingia mkataba hewa si matokeo yake unajua ni kudhulumiwa?! Hapo unakuwa umejiandaa kisaikolojia tangu mwanzo
 
Hata kama unafanya hivyo kama unadeal na mchina hali ni hiyo hiyo.

tana kusuply mchina ni wa hovyo kabisa , kila siku anatafuta supplier wapya , hupangi jambo likapangika sababu kila siku rate imebadilika kutokana na supplier mtakavyokuwa wengi
Wanawaza profit tu hawana utu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…