Kwa wafuasi wa dini nyemelezi za kigeni tu

Kwa wafuasi wa dini nyemelezi za kigeni tu

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Utafiti na uzoefu wangu umenionyesha kuwa watawala wetu wawe wa kisiasa au kiroho huwa wanajitambua kwa asili zao kwanza na dini baadae.

Mfano, Mwarabu ni mwarabu kwanza uislam unafuatilia. Mzungu ni mzungu kwanza dini inafuatia hata wakati mwingine haipo kabisa.

Kwa waswahili waliotawaliwa kiakili na kiroho utamsikia mtu akisema "mimi ni mroma" utadhani raia wa Roma. Hapa huwezi kujua kama ni mtanzania au mkazi wa Ngeme. Mwingine utamsikia "mie ni muislam na ndugu yangu ni muislam". Unashangaa.

Unataka kusema kuwa kama dada au kaka mliyezaliwa tumbo moja siyo wa dini yako si ndugu yako? Mbona hata chawa na mbuzi wanawajua ndugu zao? Je wewe binafsi huwa ni nani kwanza kabla ya yote?

Kama ni kama hao hapo juu, jua una tatizo kiakili na kiroho. Kama ni kinyume, basi uko huru na mwenye akili tosha.
 
Vijana kizazi hiki cha elfu2 mna mentally mbovu sana
 
Back
Top Bottom