Kwa waganga wasiende; Kwa manabii wasiende, mnataka waende wapi?

Kwa waganga wasiende; Kwa manabii wasiende, mnataka waende wapi?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Angalizo;

Andiko hili linaweza likawa na Lugha Kali inayoumiza, hivyo Kama wewe sio mtu wa kuhimili lugha Kali nakusihi ishia hapahapa! Au usome ukiwa chini ya uangalizi wa Wanasaikolojia na Wataalamu wa mihemko. Kama utaendelea kusoma itahesabika kuwa unahimili au upo chini ya uangalizi. Kinyume na hapo itahesabika ni ukaidi na madhara yoyote yatakuwa juu yako mwenyewe.

Tunajua watu wetu ni wajinga WA kiwango cha juu. Tunafahamu watu wetu ni masikini wa Mali na Akili. Mnataka wafanye nini? Mbona mnawasakama! Wakienda Kwa Sangoma kutafuta maisha mazuri mnapiga kelele, ooh! Washirikina, ooh! Wachawi hao, mlitaka waridhike na ujinga na ufukara wao ilhali mnawatenga na kuwabeza na Hali zao hizo.

Wakiwasikilizeni, wakasema haya, natuache kwenda Kwa Sangoma tutafute namna nyingine, basi wakasikia habari za Utajiri na baraka za ajabu, baraka za milenia, wakisikia habari za manabii na mitume wagawa Utajiri. Wakasema, sasa tutaenda huko Kwa manabii na mitume, tulisemwa Kwa Waganga WA jadi tukabezwa, sasa kumbe wapo manabii na mitume, wapo Masharifu na maimamu wakutupa Utajiri na kutuondolea misalaba yetu. Tutaenda huko nako.

Wakifika huko bado mnawasema, mnawabeza, Kwa maneno alfu ulela, mkiwaita Abunuasi mwenye ndoto za Alinacha. Mkiwaona mapoyoyo watolewa roho na moyo. Mnataka masikini na wajinga wafanyaje? Embu niambieni Leo hii! Nafahamu masikini ni Kama Swala katika Mbuga, mjinga ni Kama Digidigi tuu. Popote aendapo atawindwa na yeyote Yule.

Nafahamu shida yenu! Najua Swala amkimbiapo Simba porini akajirusha mtoni kupata msaada, Simba na fisi hupiga mayowe, huko kuna mamba, huko kuna maji weye huwezi kuogelea, toka huko uje huku porini.
Wakati mamba akishangilia Kwa ujio wa swala majini, iwe ujio wa kujiokoa na kifo cha Simba na mafisi Wabaya au kifo cha kiu akija kunywa maji.

Mamba hujitamba, njoo mwaya! Huku ni salama! Utakunywa maji. Swala atapumua Kwa afadhali kabla hajawehuka na kutoka ndukii Kwa kuona Meno makali ya mamba achanuapo mdomo wake. Hukimbia kifo majini na Kama atafanikiwa kutoka basi Mamba hupiga kelele, bora mje huku niliko kuliko kuliwa na Simba na mafisi wenye Meno makali na ulimi mbaya, ni Bora Mimi mamba sina huo ulimi wa kupiga kelele zenye dhihaka na matambo, ni lini mlimsikia mamba akitoa sauti yake. Mamba atasema hayo.

Taikon Ninajua masikini na wajinga waliumbwa kuliwa na matajiri, na Kama wasipoliwa basi kutumikishwa mpaka siku Yao ya mwisho watakapoiacha Dunia. Tena nafahamu wajinga hutumikishwa na werevu. Sikumbuki msemo wa Mbuzi WA masikini hazai. Kwani sikuhizi tutafanya Upasuaji kutokana na madaktari bingwa waliopo. Tatizo langu ni kuwa iweje Masikini na mjinga aonewe huruma na matajiri na werevu wakati akihangaika kujinasua na ufukara na Ujinga wake.

Taikon najua afanyacho masikini ndicho afanyacho Tajiri, vilevile afanyacho mjinga ndicho afanyacho Mwerevu, iweje Masikini na mjinga adhihakiwe? Masikini ataenda Kwa mganga fukara akapata ufukara ahueni, Tena mjinga ataenda Kwa Nabii mjinga akapata ujinga ahueni!
Naye Tajiri ataenda Kwa mganga Tajiri akapate Utajiri kulingana na Utajiri wake. Na Mwerevu ataenda Kwa Nabii Mwerevu akastawishwe katika werevu wake.

Unafiki Kama masikini asingekuwa masikini angekubali kwenda Kwa Sangoma fukara mwenziye, hata Taikon nisingeweza kufanya hivyo.

Acheni Masikini wazidi kukamuliwa, ninyi inawauma nini. Wakienda Kwa waganga Sawa! Wakienda Kwa akina mtume Akaba Sawa.
Wanasema mfaa maji hakomi kutapatapa. Nafahamu yapo makaburi ya Masikini ambayo hufanana na makazi Yao hapa Duniani. Halikadhalika yapo makaburi ya matajiri Ambayo hufanana na makazi Yao hapa Duniani. Na IPO Pepo ya Masikini huko waendapo

Kama ilivyo Pepo ya matajiri baada ya kuondoka kuzimu. Masikini huzalisha misukule. Na matajiri huzalisha Mandondocha.

Manabii wa masikini huchekesha na kuburudisha Nafsi za walimwengu. Ni Kama wachekeshaji fulani hivi wa madhabahuni.

Manabii wa masikini huogopa kuwaambia Mafukara ukweli kuwa Maisha ya Duniani ni Kama mbuga huko mwituni. Wapo waliozaliwa kuwatawala na kuwapa wengine, na wapo waliozaliwa kutawaliwa na kuliwa.

Wao kila muda huwafariji watu kuwa watapata Utajiri, watainuliwa, na kuwa watu wakubwa, masikini wasijue hiyo ni kejeli na dhihaka kwao kutokana na ujinga wao.

Manabii wa Matajiri huleta uchungu, hukejeli na kuwadhihaki wasakatonge.

Kila mtu apambane na Hali yake.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Angalizo;

Andiko hili linaweza likawa na Lugha Kali inayoumiza, hivyo Kama wewe sio mtu wa kuhimili lugha Kali nakusihi ishia hapahapa! Au usome ukiwa chini ya uangalizi wa Wanasaikolojia na Wataalamu wa mihemko. Kama utaendelea kusoma itahesabika kuwa unahimili au upo chini ya uangalizi. Kinyume na hapo itahesabika ni ukaidi na madhara yoyote yatakuwa juu yako mwenyewe.
Waende kwa ANUNNAKI.
 
Maada hii umevurunda hamna kitu kbs na rate 3/10

Jiwe la kikatili ambalo mpaka kesho silipingi NI lila la USIMUONEE HURUMA MWANAMKE aloooo lile ulimaliza mgogoro wote duniani..
 
Maada hii umevurunda hamna kitu kbs na rate 3/10





Jiwe la kikatili ambalo mpaka kesho silipingi NI lila la USIMUONEE HURUMA MWANAMKE aloooo lile ulimaliza mgogoro wote duniani..
ile mada nyorCo sana
team pinzani povu la Aerial
 
kwa Yesu

Mt 11:28-30 SUV​

Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
 
Angalizo;

Andiko hili linaweza likawa na Lugha Kali inayoumiza, hivyo Kama wewe sio mtu wa kuhimili lugha Kali nakusihi ishia hapahapa! Au usome ukiwa chini ya uangalizi wa Wanasaikolojia na Wataalamu wa mihemko. Kama utaendelea kusoma itahesabika kuwa unahimili au upo chini ya uangalizi. Kiny
Lugha Kali iliyozungumzwa ni ipi sasa! Si lugha ya Kawaida tu hii! Maonyo meengi, kumbe ni Staili ya kutaka Watu wengi Waisome!
 
ile mada nyorCo sana
team pinzani povu la Aerial
Ule muwa umenisaidia Sana nimekuwa bahili kutoa hata buku kwa demu Bure Bure kila nikikumbuka Uzi wa bwana mkubwa taikon hatari ..mwingine Tena wenye maajabu NI ule wa usimsaidie masikini utaambiwa una kiherehere mwache afe..[emoji1787][emoji1787][emoji1787] aloo ule wenye siupingi
 
Magazeti ya huyu jamaa yanashinda kuya soma, hivi huwa hawezi ku- summarize?? Au ana hisi hatuta mwelewa??
 
Kama mada za taikon huzielewi basi tambua sio kwa ajili yako, sio rahisi kwa kila mtu kumuelewa nguli wa fasihi Africa mashariki na kati
 
Magazeti ya huyu jamaa yanashinda kuya soma, hivi huwa hawezi ku- summarize?? Au ana hisi hatuta mwelewa??


😀😀😀😀

Mkuu watu hawafanani.
Sio kila mtu anauelewa na akili ya kuchambua mambo kwa upesi Kama wewe.

Ukilijua hili utaelewa ni Kwa nini Taikon anaandika Makala ndefu.

Hata Quran na Biblia zingeandikwa Kwa maneno machache tuu, nayo ni Mpende Bwana Mungu kwa moyo wote, kisha mpende jirani yako kama Nafsi yako. Ingetosha tuu.

Nafikiri umeelewa sasa.
 
kwa Yesu

Mt 11:28-30 SUV​

Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi



Tatizo mpaka wachawi wanasema Yesu yupo kwao.

Na hapo ndipo utata ulipo
 
Maada hii umevurunda hamna kitu kbs na rate 3/10

Jiwe la kikatili ambalo mpaka kesho silipingi NI lila la USIMUONEE HURUMA MWANAMKE aloooo lile ulimaliza mgogoro wote duniani..


Nashukuru Sana Mkuu Ndege John.

Kila mtu anamtazamo wake.

Huo unaosema nilifanya vizuri wapo waliuona nimeboronga, na huu nilioboronga wapo wanauona nimefanya vizuri.

Muhimu nashukuru Kwa kusoma na kuwa sehemu ya kazi zangu
 
Back
Top Bottom