Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Zaidi ya miaka 30, nchi ya Somalia imekuwa ni uwanja wa mapambano wa makundi yanayopingana na hakuna mwelekeo wa kupata suluhu karibuni. Ilikuwa ni nchi yenye kheri nyingi mpaka pale walipomkufuru Mungu na kufanya kiburi kwa neema walizokuwa nazo.
Marekani nayo, kwa takriban miaka 50, imekuwa ni taifa linalotamaniwa na kila mtu kuishi na kuiga mitindo ya maisha yao mpaka katika miaka ya karibuni ambapo imekuwa ikifanya kiburi na kuwatesa watu wasiokuwa na hatia.
Katika uchaguzi wao wa wagombea uraisi, ni kama wamezama kwenye matope ya kiuongozi. Wote wawili, Joe Biden wa Democratic na Donald Trump wa Republican, hawafai kuwa raisi lakini hakuna mbadala kati yao.
Joe Biden amekuwa king'ang'anizi, hataki kujiondoa kwenye uchaguzi japokuwa kumbukumbu zimempotea. Iwapo atalazimishwa kuondoka na nafasi yake kuchukuliwa na Kamala Harris, hakutokuwa na nafuu yoyote.
Donald Trump ni mtu mwenye laana za kila aina na kashfa za kisiasa na kijamii. Joe Biden ameweka wazi kuwa ni fashisti na lazima asitishwe. Mtu huyu ana laana za uzinifu na wizi wa nyara za serikali. Zaidi ya yote ana mdomo unaotamka mambo kiholela na kuchochea chuki dhidi yake. Ndio kiongozi pekee aliyejifanya jabari na kuamua kuvunja heshima ya Jerusalem kwa Wapalestina na Waislamu kwa ujumla.
Kupigwa risasi kwake, japo ametobolewa sikio tu na kuchuruzikiwa damu usoni, lakini pigo hilo ni pigo ambalo limeijeruhi Marekani yote na itakuwa ni kidonda kisichosikia dawa.
Machafuko ndani ya Marekani katika wakati ambao imeshadhoofika ni kitu endelevu na hilo ni pigo takatifu kutoka kwa muumba wa ulimwengu kwa taifa ambalo limeongoza kufanya jeuri ya mali na elimu ambavyo walipewa dhamana tu.