charger
JF-Expert Member
- Nov 21, 2010
- 2,320
- 1,371
Habari ya mchana,asubuhi etc wana jf.Naamini Mola anaendelea kuwapa uhai japo wakati mwingine mnasahau kumshukuru na kutubu kwa kuvunja amri ya 7 kwa kujitambulilisha jukwaani kwa majina yasiyokuwemo kwenye vyeti vyenu vya kuzaliwa.
Tuachanane na hayo,hoja yangu leo ni kuhusu milio ya magari na wasafiri.Yapo magari aina nyingi kama scania,fiat,Nissan march,Toyota hilux,Suzuki escudo,Nissan murrano,Leyland na mengine mengi.Ishu inakuja wakati wa safari kuna magari yanamlio mkubwa tangu mwanzo wa safari hadi mwisho,mengine hata kama hayana mzigo mkubwa yanalia kama yana tani 200 za sukari,mengine yanalia kama vile yapo na speed 160km/hr kumbe unaweza kukuta ni speed 20 tu.Mengine yanaunguruma kama simba,mengine yanatoa sauti kama vile gear imeingizwa bila kukanjangwa clutch,mengine mlio kama mafla zimepasuka,mengine kama vile yanatembelea rim.
Namengine yenyewe ni kimya kimya tu liwe na mzigo ,kona kali,mteremko mkali lenyewe ni kimya tu.Na mengine likiwashwa tu basi wapangaji woooote watajua baba,mama,dada au kaka flani kaanza safari
Swali ni hivi,je sauti na mlio wa gari au ukimya wa gari wakati wa safari unauhusiano wowote katika kumpa hamasa au kumwondolea raha msafiri?
Nawasililisha hoja kwa yeyote atakaye husika.